LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 23, 2024

BODI YA STAKABADHI YA GHALA YAELEZA UFANISI WAKE MBELE YA KAMATI YA BUNGE YA VIWANDA

 

Mwenyekiti wa Kamati Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Kilimo, Deodatus Mwanyika akiongoza kikao wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Asangye Bangu akielezea kuhusu utendaji, mafanikio na changamoto zinazoikabili bodi hiyo, wakati wa kikao na wajumbe wa kamati hiyo katika moja ya kumbi za mikutano za Bunge jijini Dodoma Oktoba 23, 2024.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mwanyika akisikiliza kwa makini wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Asangye Bangu akielezea kuhusu utendaji, mafanikio na changamoto zinazoikabili bodi hiyo, 

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Asangye Bangu akielezea kuhusu utendaji, mafanikio na changamoto zinazoikabili bodi hiyo wakati wa kikao na wajumbe wa kamati hiyo katika moja ya kumbi za mikutano za Bunge jijini Dodoma Oktoba 23, 2024.

Bodi hiyo ambayo iko chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara, kazi yake kuu ni kusimamia na kuhamasisha matumizi ya mfumo wa stakabadhi ghalani unaohakikisha usawa na uendelevu wa upatikanaji wa mikopo na mifumo ya masoko.

Dhamira yake ni Kuchochea maendeleo ya uchumi wa bidhaa na wamiliki wa ghala kwa kusimamia ghala na kuhakikisha usawa na upatikanaji endelevu wa huduma za fedha, mifumo ya masoko ya mazao na bei ya ushindani.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Suleiman Jaffo akifafanua jambo wakati wa kikao hicho.
Wabunge ambao ni wajumbe wa kamati hiyo wakiwa makini kusikiliza uwasilishwaji huo.


Baadhi ya maafisa wa wizara hiyo na bodi hiyo wakiwa katika kikao hicho.
Waziri Jaffo akiandika baadhi ya mambo muhimu.
Waziri Jaffo akiwa na viongozi wa wizara na bodi wakiondoka baada ya kikao kumalizika.


IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA

MHARIRI

BLOG YA TAIFA YA CCM

0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages