Na Victor Makinda. Morogoro.
Adha ya waliyokuwa wakiipata wateja kusubiri muda mrefu baada ya maombi ya kuunganishiwa umeme imefika mwisho mkoani Morogoro.
Meneja wa TANESCO mkoa wa Morogoro, Mhandisi Fadhili Chilombe, amesema kuwa kuanzia sasa mteja ataye wasilisha ombi la kuunganishiwa umeme, itachukua siku saba tu kupatiwa huduma hiyo muhimu.
Mhandisi Chilombe ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro, kuelezea wiki ya huduma kwa wateja na namna TANESCO mkoani humo ilivyojipanga kuboresha huduma.
Msikilize https://www.youtube.com/watch?v=bVVf8I24CJM
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇