LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 10, 2024

DK. NCHIMBI ASISITIZA KUDUMISHA AMANI

 Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, amesema amani na mshikamano wa Watanzania unapaswa kuwa mojawapo ya vipaumbele kwa kila Mtanzania. 


Balozi Nchimbi amesema kuwa wasisi wa Taifa la Tanzania na wazee walifanya kazi kubwa katika kuweka misingi ya kulinda na kutunza amani ya nchi, wakitumia hekima na uzoefu ili kuhakikisha kuwa jamii ya Watanzania inakuwa na mshikamano siku zote. 


“Ni jukumu letu sasa kuendeleza amani hiyo na thamani yake kwa ajili ya vizazi vijavyo. Ni muhimu kutunza umoja wetu na kushirikiana kwa pamoja. Tunapaswa kudumisha na kujenga mazingira ya amani na ushirikiano. Umoja ni nguvu.”


“Hatupaswi kukubali kuharibiwa umoja wetu. Tunapaswa kufanya kazi pamoja ili kulinda amani na kutatua tofauti zetu kwa njia ya mazungumzo na kuelewana. Umoja wetu ni msingi wa nguvu na amani,” amesema Balozi Dk. Nchimbi. 


Balozi Nchimbi ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa eneo la Tinde mkoani Shinyanga, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ndani ya mkoa huo, akiongozana na Katibu wa NEC-Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu Amos Makalla pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndugu Rabia Abdalla Hamid 

đź—“️09 Octoba 2024.

đź“ŤTinde, Shinyanga.



Dk. Nchimbi na viongozi wengine wakiingia kwenye Uwanja wa mkutano.
Dk. Nchimbi akiteta jambo na mmoja wa mabinti wa eneo hilo.
Katibu wa Itikadi,Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla akihamasissha wananchi.

Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndugu Rabia Abdalla Hamid akizungumza katika mkutano huo.

Mbunge wa Solwa, Ahmed Salum akielezea jinsi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025  ilivyotekelezwa katika jimbo hilo.

Ilikuwa ni furaha ya aina yake.


Sehemu ya umati wa wananchi waliofika kumsikiliza Dk. Nchimbi.




 Ngoma za utamaduni zikitumbuiza.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages