LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 6, 2024

SHIRIKIANENI NA CCM NDIYO CHAMA CHENYE UWEZO NA DHAMIRA KUONGOZA NCHI - NCHIMB


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amesema hadi sasa hakuna chama kingine cha siasa, tofauti na CCM, kinaweza kuaminiwa kuwa mbadala wa CCM katika kuongoza nchi.

Hivyo amewasisitiza Watanzania kuendelea kushirikiana na CCM kwani ndiyo chama chenye uwezo na dhamira ya kuongoza nchi kwa maslahi ya wananchi na taifa letu.

Balozi Nchimbi ameyasema hayo leo tarehe 6 Oktoba, 2024, alipokuwa akizungumza na wananchi wa Lamadi, Wilaya ya Busega, mkoani Simiyu, ambapo pia amewapongeza kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mapokezi yake, I ikionesha wazi mapenzi yao makubwa kwa CCM.

"Shirikianeni na Chama Cha Mapinduzi ambacho kimeonesha uwezo na dhamira ya kuongoza nchi. Sisi hatuna viongozi wa kuongoza miaka 40 bila kubadilika. Tunabadilika badilika na ndiyo mana CCM imekuwa chama kijana kuliko vyote. Vyama vya upinzani bado sana vinahitaji kukua na sio kuongoza. Tuendelee kuwalea ni watoto wa mwisho hadi watakapokua zaidi, labda miaka 50 ijayo.

Dkt Nchimbi ameongozana na Katibu wa NEC-Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu CPA Amos Makalla na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndugu Rabia Abdalla Hamid.


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akizungumza na wananchi wa Lamadi, Wilaya ya Busega, mkoani Simiyu, leo tarehe 6 Oktoba, 2024


Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndugu Rabia Abdalla Hamid, akizungumza na wananchi wa Lamadi, Wilaya ya Busega, mkoani Simiyu, leo tarehe 6 Oktoba, 2024

Katibu wa NEC-Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu CPA Amos Makallai, akizungumza na wananchi wa Lamadi, Wilaya ya Busega, mkoani Simiyu, leo tarehe 6 Oktoba, 2024

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages