LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 6, 2024

HODI SIMIYU, NCHIMBI AKIANZA ZIARA YA SIKU 3

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi (aliyesimama juu ya gari la kijani) akizungumza na wananchi wa Lamadi, Wilaya ya Busega, Mkoa wa Simiyu, leo tarehe 6 Oktoba 2024, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu mkoani humo. Kushoto aliye juu ya gari  jeupe ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Amos Makalla.


Balozi Nchimbi ambaye ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Amos Makalla na Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (Suki), Ndugu Rabia Hamid Abdalla, ameanza ziara mkoani Simiyu kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020 - 2025, kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi, kukagua uhai wa Chama kuanzia ngazi ya mashina na pia kuhamasisha wananchi kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, utakaofanyika mwezi Novemba, mwaka huu.

Akihutubia wananchi.
Dkt. Nchimbi akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Kenani Kihongosi (kulia) pamoja na viongozi wengine.


Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (Suki), Ndugu Rabia Hamid Abdalla akitoa somo.

 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages