LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 6, 2024

PRO. NDAKIDEMI AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUJITOA KIMASOMASO KUBORESHA SEKTA YA ELIMU NCHINI

 Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi  ameipongeza  Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada kubwa zinazofanyika kwenye kuwekeza katika sekta ya elimu nchini. 

Prof Ndakidemi ameyasema hayo tarehe 5 Oktoba, 2024 alipokuwa Mgeni rasmi kwenye Mahafali ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Masoka iliyopo Halmashauri ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.

 Aliipongeza sana Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na sekta ya elimu kwa jamii hapa nchini.

 "Kwa kutambua umuhimu wa sekta ya elimu, serikali  imejitoa kimasomaso kubeba gharama za kuwekeza kwenye miundombinu ya shule ikiwemo ujenzi wa madarasa, maabara, mabweni, nyumba za waalimu, kutoa vifaa vya kufundishia na  kuongeza ajira kwa walimu," alisema na kuongeza

  ...Vilevile, serikali imeendelea kutoa elimu bila ada kwa watoto wote kuanzia shule za msingi hadi kidato cha sita, jambo ambalo  limeongeza chachu ya kukuza na kuhamasisha jamii kuipenda elimu."

Mbunge aliipongeza serikali kwa uwekezaji mkubwa katika Shule ya Sekondari Masoka ambapo hivi karibuni wameipandisha hadhi na kuwa Masoka High School, katika kufanikisha hili, Serikali imetoa shilingi milioni 393.6 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa manne, mabweni mawili na matundu 16 ya vyoo.

Katika hafla hiyo, Profesa Patrick Ndakidemi  aliwapongeza Walimu wa Shule ya Sekondari Masoka (wakiongozwa na bodi ya shule na Mwalimu Mkuu Ahmed Litinji) kwa uchapakazi hodari kwani  wamekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza majukumu yao ya kutoa elimu bora kwa wanafunzi, jambo ambalo limeifanya Sekondari ya Masoka kuwa shule inayoheshimika kitaaluma katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro na hapa nchini. 

Katika kukabiliana na changamoto ya michezo hapo shuleni, Mbunge alitoa fedha taslimu kutengeneza magoli katika viwanja vya michezo, mipira na seti ya jezi.


Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu wakati wa mahafali ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Masoka iliyopo Halmashauri ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
Prof. Ndakidemi akiwa na mmoja wa wanafunzi.

Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika sherehe za mahafali hayo.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages