LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 14, 2024

NHIF WALA KIAPO CHA KUWATUMIKIA WATANZANIA KWA UADILIFU

 Na Mwandishi Wetu, NHIF

Jumla ya watumishi 410 wa Mfuko  wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), wamekula kiapo cha kutunza siri  na kuwatumikia Watanzania kwa weledi na kwa kufuata maadili ya Utumishi wa Umma.


Zoezi hili limefanyika siku ya Jumamosi Tarehe 12 Oktoba  na Jumapili Tarehe 13 Oktoba,2024 Jijini Dodoma wakati wa mafunzo elekezi kwa Maofisa Udhibiti Ubora, Maofisa Madai na Maofisa Wanachama.


 Akizungumza katika mafunzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Dkt. Irene Isaka amesema kuwa umuhimu wa mafunzo hayo na kiapo ni kuwakumbusha Watumishi wa Mfuko kuwa wana wajibika kwa Wanachama, Wadau wa Mfuko na wananchi kwa ujumla.

 Aliwakumbusha dhamana kubwa waliyopewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo wanatakiwa kuzingatia Sheria, Kanuni,  miongozo ya Sera, Sheria, kanuni na taratibu na kutekeleza majikumu yao kwa uadilifu mkubwa. 


Aliwakumbusha kwamba tuache kufanya kazi kwa mazoea tunapowapa huduma wanachama wetu na wadau mbalimbali. Alihimiza kuwa wabunifu na kutumia mifumo ili kutatua changamoto zinazokabili Mfuko na Sekta kwa ujumla hususani katika kipindi hiki ambacho tunaanza utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote.


“Ni jukumu letu sisi kuhakikisha  tunawahudumia wanachama na wadau kwa weledi mkubwa na kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma na ndio maana tunakula kiapo hiki kinachotutaka pia kutunza siri za Serikali," amesema Dkt. Isaka.


Alitumia fursa hiyo kuwahimiza watumishi kuweka nguvu kubwa katika uelimishaji umma  kuhusu huduma zinazotolewa na Mfuko ili kujenga uelewa kwa wadau na Umma kwa ujumla. 


Katika kikao kazi hicho. Kundi la Afisa uanachama walielekezwa namna ya kutumia Mfumo wa uandikishaji wanachama, kupokea michango pamoja na namna ambayo wanachama na wadau wanavyoweza kutuma malalamiko yao kidigitali. Watumishi hao walipata mafunzo ya namna ya kutambua viashiria vya udanganyifu kwa wanachama na waajiri na hatua stahiki za kuchukua 


 Kwa upande mwingine kundi la  Maafisa ubora na Maafisa Madai walielekezwa namna ya kutumia Mfumo wa kuchakata madai ili kulipa kwa wakati. Vile vile walipata mafunzo ya namna ya kutambua viashiria vya udanganyifu kwa watoa huduma na hatua stahiki.


*Bima ya Afya kwa Wote, jiunge sasa*

 

Mkurugenzi Mkuu wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dkt. Irene Isaka akizungumza wakati wa mafunzo  elekezi kwa Maofisa Udhibiti Ubora, Maofisa Madai na Maofisa Wanachama wa mfuko huo jijini Dodoma.

Sehemu ya watumishi wa mfuko huo wakiwa katika mafunzo hayo.




No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages