LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 31, 2024

MFUKO WA MAJI WA TAIFA WAELEZA MAFANIKIO YAKE MIAKA MITATU YA RAIS DK. SAMIA, WATOA MIKOPO YA BILIONI 5.4 KWA MAMLAKA ZAMAJI

Na Bashir Nkoromo, Blog ya Taifa ya CCM

Mfuko wa Maji wa Taifa umesema hadi kufikia Julai 2024, ulikuwa umetoa mikopo ya jumla ya sh. Bilioni 5.3, kwa Mamlaka za Maji mijini na vijijini, huku maombi ya mikopo ya thamani ya sh. Bilioni 13 yakiwa yanaendelea kuchakatwa.


Hayo amesemwa leo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo Wakili Haji Mandule, akieleza mafanikio yaliyofikiwa na Mfuko huo katika kipondi cha uongozi wa Rais wa Awamu ya Sita Dk. Samia Suluhu Hassani.


Ameeleza mafanikio hayo, katika kikao kazi baina ya uongozi wa Mfuko huo na Wahariri wa habari zaidi ya 50, kilichoratibiwa na Ofisi ya msajili wa Hazina na kufanyika jijini Dar es Salaam.


Katika Kikao kazi hicho ambacho Ofisi Msajili wa Hazina ilikiandaa kutoa nafasi kwa Mfuko huo uuleleze umma utendaji na mafanikio yake, Afisa Mtendaji Mkuu huyo, alieleza mafanikio mengi ambayo kulingana na kutokuwa na muda mrefu tangu mfuko huo uanze kazi serikali inapaswa kupongezwa kuuanzisha.


Kuelewa kwa undani, mafanikio hayo tafadhali soma taarifa hii kamili iliyotolewa na Afisa Mtendaji Mkuu kwenye kikao hicho.👇

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages