Katibu wa NEC-Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu Amos Makalla ,akizungumza na maelfu ya Wananchi akihitimisha Ziara ya Siku 7 ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Emmanuel Nchimbi kwenye mikoa ya Simiyu na Shinyanga.
.......................................
Katibu wa NEC Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu Amos Makalla leo akizungumza na Mamia na Maelfu ya Wananchi wa Shinyanga amesema Chama cha mapinduzi kwenye Kuhamasisha wamefanya kazi kubwa kwani Chama na Jumuiya zake pamoja Viongozi walikuwa wanapishana kwenye Kuhamasisha sasa anashangaa upande wapili wanahangaika eti Serikali ihamasishe wenyewe wakiwa wapo bize na Uchaguzi wa kanda ni kama wameingia uwoga.
"Mimi nimeshuhudia namna ambavyo Chama cha mapinduzi na Jumuiya zake na Viongozi wake wa ngazi zote jinsi tulivyokuwa mstari wa mbele katika Kuhamasisha Wananchi Kujiandikisha katika daftari la Wakazi.Wenzentu wameingia ubaridi wana wasiwasi wakushindwa Uchaguzi huu kwani hawajajipanga kwani sasa wanahangaika na Uchaguzi wa kanda "
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇