Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Emmanuel Nchimbi, akizungumza na maelfu ya Wananchi akihitimisha Ziara yake ya Siku 7 kwenye mikoa ya Simiyu na Shinyanga akiwa ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu Amos Makalla pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndugu Rabia Abdalla Hamid.
..................................
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi leo tarehe 11 Octoba 2024 akiwa akizungumza na Wananchi wa Shinyanga Mjini ametatua kero ya Wananchi ya uhitaji wa Kituo cha Afya Kata Ibadakuli hivyo amemuelekeza Waziri wa Tamisemi Mohammed Mchengerwa kuhakikisha Kituo cha Afya Ibadakuli kinajengwa kwa ajili ya Kusaidia Wananchi kupata huduma za Afya.
"Nichukue nafasi hii kumuelekeza Waziri wa Nchi Tamisemi, Mohammed Mchengerwa Popote alipo, hili ni agizo la Chama cha Mapinduzi (CCM) ahakikishe kuwa Kituo cha Afya Ibadakuli kinaanza Kujengwa mara moja, natambua yeye ni miongoni mwa Mawaziri Wasikivu na Wachapakazi kwenye Serikali" amesema Dkt Nchimbi.
Dkt Nchimbi ametoa agizo hilo leo Oktoba 11, 2024 wakati akihitimisha Ziara yake ya Siku 7 kwenye mikoa ya Simiyu na Shinyanga akiwa ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu Amos Makalla pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndugu Rabia Abdalla Hamid.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇