Singida.
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge
na Uratibu, Mhe. William Lukuvi amefungua rasmi Maonesho ya Saba ya
Mifuko na Programu za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Mkoani Singida ambayo
yanaratibiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC)
Wakati
wa ufunguzi wa maonesho hayo, Mheshimiwa Lukuvi amesema kuwa maonesho
hayo yatafungua fursa za Kiuchimi kwa wafanyabiashara, wakulima na
wafanyabiashara wa Singida na Mikoa ya Jirani.
Waziri
Lukuvi Aliongeza kuwa, Maonesho hayo yatawezesha wananchi kupata huduma
za uwezeshaji ikiwemo mitaji, mikopo nafuu, dhamana za mikopo, vifaa,
mashine au mitambo, urasimishaji ardhi,urasimishaji biashara, huduma za
msimbomilia, ujuzi, ithibati ya bidhaa, huduma za sheria, huduma za
ushirika, huduma za ushauri wa kitalaam, elimu rasmi na elimu ya ufundi
stadi, kuunganisha wananchi na fursa,na ukaguzi wa bidhaa.
Mhe.
Lukuvi alibainisha kuwa, Maonesho hayo ni muhimu kwa kuwa yanakutanisha
wadau mbalimbali wa uwezeshaji wakiwemo, Wizara, Mikoa, Halmashauri;
Taasisi zinazosimamia Mifuko na Programu za Uwezeshaji, Taasisi za
Fedha, Wafanyabiashara, Kampuni, Taasisi za Elimu na Tafiti, Wakulima,
Wafugaji,na Wajasiriamali.
Aliongeza
kuwa, Maonesho hayo yana lengo la kuhakikisha kuwa washiriki
wanabadilishana ujuzi, maarifa, uzoefu na teknolojia mbalimbali ambazo
zinatumika katika kukuza ushiriki wa wananchi katika shughulli za
kiuchumi.
“Nina imani kuwa, Maonesho haya yatatoa fursa nyingi kwa wananchi wa Mkoa wa Singida na Mikoa mingine.” Alisisitiza
Akiongea
kwa Niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge naa
Uratibu), Dkt. Jim Yonazi, Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi, Bw. Condrad Milinga amesema kuwa
pamoja na maonesho hayo kutoa fursa mbalimbali kwa wajasailiamali,
wananchi pia watapata mafunzo na ujuzi kuhusu masuala mbalimbali kutoka
kwa Washiriki wa Maonesho na kutoa wito kwa wananchi kutembelea maonesho
hayo.
Kwa
Upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi
kiuchumi (NEEC), Bi Beng’ Issa amesema kuwa kwa miaka mingi Serikali
imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali za kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa
lengo la kujenga uchumi na kuwaondoa wananchi katika umaskini.
“Juhudi
hizo ni pamoja na kuanzisha mifuko na program za uwezeshaji mbalimbali
kwa lengo la kutoa mikopo au dhamana ya mikopo kwa wananchi kwa masharti
nafuu, kutoa ruzuku pamoja na kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi ili
waweze kukopesheka au kuhudumiwa na wadau wengine.” Alibainisha
Aliendelea
kufafanua kuwa, mpaka sasa Baraza linaratibu Jumla ya Mifuko ya
Uwezeshaji na Programu 72 ambayo 62 ipo Serikalini na 10 ipo Sekta
binafsi, hivyo Lengo kuu la Maonesho haya ni kutoa uelewa wa fursa za
Mifuko kwa Wananchi ambapo ilionekana mifuko mingi haifahamiki kwa
wananchi hivyo kuchelewesha kufikisha huduma za uwezeshaji kwa wananchi.
Maonesho
hayo ya siku Saba yaliyofunguliwa leo Mkoani Singida yana Kaulimbiu
inayosema “Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Unufaike na Fursa za
Uwezeshaji”
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇