Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Simbachawene leo amemtembelea nyumbani kwake Kawe jijini Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dk. Jakaya Kikwete, na kufanya mazungumzo
Katika mazungumzo hayo, Simbachawene amefikisha salaam za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye ameahidi kuendelea kuwa pamoja na Viongozi Wakuu Wastaafu wa Kitaifa kwa maendeleo ya taifa.
Simbachawene amesema Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ina jukumu la kutunza Viongozi Wakuu Wastaafu Kitaifa na Wenza wao, hivyo yuko tayari kuendelea kutekeleza jukumu hilo alilopewa na Rais Dk. Samia kwa ufanisi.
Dk. Kikwete amemshukuru Simbachawene kwa ujio huo na kupongeza utaratibu uliopo wa kuwatembelea Wiongozi Wakuu Wastaafu wa Kitaifa kwa kuwa unawapa faraja, unaonesha thamani na mchango wao kwa maendeleo ya taifa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene akizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete, nyumbani kwake Kawe Jijini Dar es Salaam, leo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇