Na Bashir Nkoromo, CCM Official Blog
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, imepongezwa kwa kutouchakachua mradi wa ujenzi wa shule mpya ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza Richard Mgana inaoutekeleza katika eneo la Kigogo, jijini Dar es Salaam, kwa gharama ya sh. Bilioni 1.158.
Imepongezwa pia kwa 'kuijiongeza' na kujazia fedha zake, baada ya kuona fedha ilizokuwa imetengewa na serikali sizingeweza kukamilisha aina ya ujenzi inaotaka, kwa kuwa zililenga ujenzi msambao wakati Manispaa hiyo ilihitaji ujenzi wa aina ya ghorofa kutokana na ufinyu wa eneo.
Pongezi hizo zimetolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo ilipokagua ujenzi wa shule hiyo, leo Septemba 10, 2024, ikiongozwa na Mwenyekiti wake Husna Sekiboko na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Elimu, Utamaduni na Michezo Omari Kipanga ambaye ni Mbunge wa Mafia.
"Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa napenda kuipongeza Halmashauri ya Kinondoni, kwanza kwa kutochakachua katika utekelezaji wa mradi huu na pia niwapongeze kwa kujiongeza, na kujazia fedha za kukamilisha mradi.
Wakati tunakagua mradi huu kwa kweli nilivyouona inaonekana kabisa hakuna uchakachuaji uliofanywa, maana baadhi ya mahala pengine unakuta ukiuangalia mradi unaona kabisa kuna kauchakachuaji, utekelezwaji wake haulingani kabisa na thamani ya fedha.
Lakini pia niwapongeze kwa namna viongozi wa Halmahsuri hii, mlivyojiongeza baada ya kuona kuwa fedha ziliotengwa hazitatosha aina ya ujenzi mnaouhitaji mkaamua kuongeza fedha kutoka kwenye mapato ya ndani ya Halmashauri yenu. Hongereni sana viongozi wa Manispaa hii", akasema Mjumbe wa kamati hiyo, Mbunge wa Ulyankuru Rehema Kiigilla.
Akisoma taarifa ya maendeleo ya mradi huo, iliyoandaliwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Hanifa Hamza, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Hanifa Manase Urio, alisema Aprili 2023 Shule Mama ya Msingi Mapinduzi ilipokea Sh. milioni 475..3 kwa mfumo wa ''Force Account'' kwa ajili ya kutekeleza mradi wa shule ya mikondo miwili na miundombinu iliyopaswa kujengwa ni vyumba 16 vya madarasa, matundu 24 ya vyoo, jengo la Utawala na kichomea taka.
Alisema kutokana na ufinyu wa eneo Halmashauri ilifanya usanifu wa jengo la ghorofa na ikaomba kibali cha kutekeleza mradi kwa muundo wa ghorofa lenye thamani ya sh. Bilioni 1.158 baada ya ombi kukubaliwa na OR-TAMISEMI, halmashauri iliahidi kuongeza sh. Milioni 682.754.
Mwalimu huyo alisema Mradi ulianza kutekelezwa Agosti 4, 2023 na hadi sasa umefikia asillimia 90 kukamilika na miundombinu inayojengwa ni vyumba 18 vya madarasa, matundu 36 ya vyoo, Jengo la Utawala na kichomea taka ikiwa ni ongezeko la vyumba viwili vya madarasa, na matundu kumi ya vyoo kulingana na vyongozo wa BOOST uliokuwa umetolewa.
Alitaja shugjuli zilizosalia ili mradi kukamilika kuwa ni kupaka rangi jengo lote, kupiga chipping nyuma ya jengo, kuweka milango madarasa 12 na vyoo 20, kuweka malumalu madarasa 6, vyoo matundu 20 na baraza sakafu ya kwanza na ya pili.
Alitaja manufaa yatakatopatikana kukamilika kwa shule hiyo ni pamoja na kupunguza msongamano kwenye shule jirani za Mapinduzi na Gilman Rutihinda.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo Husna Sekiboko (Watatu kushoto), akiongoza Wajumbe wa Kamati hiyo kukagua ujenzi wa shule mpya ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza Richard Mgana leo Septemba 10, 2024, Wanne ni Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge.Naibu Waziri wa Elimu, Utamaduni na Michezo Omari Kipanga akizungumza wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge kupokea taarifa ya Utekelezwaji wa Mradi wa ujenzi wa shule hiyo.Baadhi ya Washiriki wakiwa kwenye kikao hicho.
Naibu Waziri akifanya utambulisho.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo Husna Sekiboko akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwalimu Mkuu Hanifa Manase Urio akisoma taarifa ya Utekelezaji na maeleo ya mradi huo iliyoandaliwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Hanifa Hamza. Mbunge 'Babu Tale' akizungumza kwenye kikao hicho.
Diwani wa Kata ya Kigogo Richard Mgana (kulia), akizungumza kwenye kikao hicho.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge akizungmza kwenye kikao hicho.
DC Mtambule akizungumza kwenye kikao hicho.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Hanifa Hamza akizungumza kwenye kikao hicho.
Mjumbe wa Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge, Mbunge wa Ulyankuru, Rehema Kiigilla akizungumza kwenye kikao hicho.
Mbunge Bidyanguze akifurahia jambo na Meya Songoro Mnyonge wakati wakitoka ukumbini baada ya kikao hicho.
Mweneyekiti wa Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge Husna Sekiboko akiongoza Wajumbe kutoka ukumbini baada ya kikao hicho.
DC Mtambule na Meya Songoro Mnyonge wakijadili jambo na Mkurgenzi Hanifa baada ya kutoka ukumbini mwishoni mwa kikao hicho.
Moja ya chumba cha darasa katika shule hiyo inayojengwa.
Sehemu ya muonekano wa shule hiyo inayojengwa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇