LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 23, 2024

UWANJA WA MAJIMAJI WAFURIKA WATU KUMSIKILIZA RAIS SAMIA

 Songea, Ruvuma.

Katika hali ya hamasa kubwa, umati mkubwa wa wananchi wa Mji wa Songea umejitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Majimaji, kumshuhudia na kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 23 Septemba 2024  katika kilele cha Tamasha la Tatu la Kitaifa la Utamaduni, lililoandaliwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, mkoani Ruvuma.

Mhe. Rais Dkt. Samia ni mgeni rasmi wa tamasha hilo, lililojikita katika kuonesha na kusherehekea utajiri wa urithi wa kitamaduni wa Tanzania. 

Kabla ya hotuba yake, Rais alipata fursa ya kutembelea mabanda ya maonesho ya utamaduni, ambapo alijionea kazi mbalimbali za sanaa na utamaduni, na hata kushiriki kucheza mchezo wa bao, jambo lililowafurahisha wananchi na wasanii waliokuwepo.

Shughuli hiyo inaendelea kwa shamrashamra, huku wananchi wakionesha shauku na furaha kubwa kwa ziara ya Rais katika eneo hilo, likiwa na umuhimu mkubwa kwa historia na utamaduni wa taifa.

Umati mkubwa wa wananchi wa Mji wa Songea umejitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Majimaji, kumshuhudia na kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 23 Septemba 2024  katika kilele cha Tamasha la Tatu la Kitaifa la Utamaduni, lililoandaliwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, mkoani Ruvuma.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,  akiwasalia wananchi waliofurika kumsikiliza kwenye Uwanja wa Maji Maji Septemba 23, 2024  katika kilele cha Tamasha la Tatu la Kitaifa la Utamaduni, lililoandaliwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, mkoani Ruvuma. Kutoka kushoto ni Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed.

                                  

Rais Samia akipitia hotuba yeke kabla ya kuanza kuhutubia.

Sehemu ya umati wa watu waliofurika kwenye uwanja huo wa Maji Maji.



 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages