LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 23, 2024

RAIS SAMIA ALAKIWA KWA SHANGWE NA VIGELEGELE, AKIANZA ZIARA RUVUMA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Samia Suluhu Hassan, amewasili Mkoa wa Ruvuma na kupokelewa kwa nderemo na vifijo, wakati akianza ziara ya kikazi mkoani humo, leo Septemba 23, 2024.


Wananchi wa Mji wa Songea, wakiongozwa na viongozi wa Chama na Serikali, walijitokeza kwa wingi kumpokea Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, katika Uwanja wa Ndege wa Songea, kwa shangwe na vigelegele.

Baada ya kuwasili uwanjani hapo, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, alipata fursa ya kukagua na kupewa taarifa ya ukarabati na maboresho ya Uwanja wa Ndege wa Songea, kutoka kwa Waziri wa Ujenzi, Ndugu Innocent Bashungwa na watalaam kutoka wizarani.

Mhe. Rais Samia kabla ya kuondoka uwanjani hapo kuendelea na ratiba za shughuli nyingine katika siku ya kwanza ya ziara yake katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Ruvuma, pia amepata fursa ya kutazama vikundi mbalimbali vya burudani, vikiongozwa na vikundi vya ngoma za asili za Mkoa wa Ruvuma.

Baadae leo jioni, Mhe. Rais Samia anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la 3 la Kitaifa la Utamaduni, ambalo mwaka huu limefanyika mkoani Ruvuma.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Songea kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi Mkoani Ruvuma tarehe 23 Septemba, 2024.

Akisli,iama ma viongozi mbalimbali waliofika kumlaki.


Baadhi ya viongozi waliofika kumlaki Rais Samia.


Rais Samia akiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za asili. 




Wananchi wakishangilia wakati wa mapokezi hayo.





No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages