Na Bashir Nkoromo, Blog ya Taifa ya CCM
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam Songoro Mnyonge ameomba wadau wa usafi Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) kutoa msaada wa kuweka vizuizi vya taka ngumu kwenye mito inayoingiza maji baharini ili kutunza mazingira.
Pia amewataka wafanyabiashara katika eneo la ufukwe wa Coco Beach, kuzingatia usafi wakati wa shughuli zao ili kutunza mazingira ya usafi katika ufukwe huo.
Mstahiki Meya amesema hayo, leo Agosti 31, 2024 wakati Wadau mbalimbali na wananchi walipofanya usafiri katika ufukwe wa Coco Beach, ikiwa ni kutekeleza azma ya Manispaa hiyo ya Kinondoni kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Manispaa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.
"Katika Manispaa yetu tuna mito 19 inayoingiza maji badaharini, TCC tunaomba mtusaidie kuweka vizuizi vya taka ngumu kwenye hata baadhi ya mito hii ili kuweza kunusuru mazingira ya bahari yasichafuke.
Tunajua mmeshafanya kwenye mto mmoja wapo katika Manispaa hii, lakini tusaidieni katika hili japokuwa isiwe mito yote, lakini mkifanya hivi mtakuwa mmesaidia sana", alisema Mstahiki Meya ambaye alimuwakilisha Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, ambaye alipata udhuru wa kutofika Coco Beach kushiriki usafi kama iliyokuwa imepangwa.
Kuhusu Wafanyabiahara Coco Beach Mstahiki Meya aliwataka kuhakikisha taka hazizagai hovyo wanapofanya shughuli zao ili kuhakikisha eneo hilo linakuwa safi wakati wote.
"Ninyi wafanyabishara hapa mna vikundi vyenu, kwa hiyo naagiza mshirikiane kuhakikisha mnasimamiana kudhibiti utupaji hovyo wa taka ili mazingira yawe safi.
Sanjari na agizo hilo, Mstahiki Meya aliagiza vifaa mbalimbali vilivyotolewa na wadau (TCC) kuhakikisha wanavitunza na kuvitumia kwa lengo lililokusudiwa na kuonya kuwa waliokabidhiwa wasivipeleke vyumbani vifaa hivyo. " Naagiza vifaa hivi vikawekwe vilikokusudiwa msivipeleke vyumbani kwenu, mimi na wenzangu tutakuwa mara kwa mara kupita kukagua kama vipo na vinatumika", alisema Mstahiki Meya.
Katika usafishaji huo, wadau TCC na wananchi walifanya usafiri kuanzia saa 12 asubuhi wakiongozwa na Mstahilki Meya Songoro Mnyonge, Viongozi na baadhi ya Wafanyakazi wa TCC wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCC Pic Takashi Araki na Balozi wa Japan hapa nchini Yusushi Misawa na Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni hiyo Patricia Mhondo.
Wadau wakifanya usafi katika Ufukwe wa Coco Beach Agsosti 31, 2024,
Wadau Daniel Gwaselya na Balnaba Ndalima wakifanya usafi eneo hilo la Coco Beach
Mkurugenzi Mkuu wa TCC Pic Takashi Araki (kulia) akisaidiana na Kijana wake kufanya usafi Coco Beach.
Mwenyekiti wa Bodi ya TCC Paul Makanza akikabidhi vifaa vya usafi kwa Mstahiki Meya Songoro Mnyonge, baada ya shughuli ya usafi Coco Beach..
Mstahili Meya Songoro Mnyonge akifurahi baada ya kukabidhiwa vifaa.
Akiinua juu pipa la kuhifadhi taka baada ya kukabidhiwa,
Akiinia chombo la kubebea taka baada ya kukabidhiwa.
Mstahiki Meya akimkabidhi reki, Balozi wa Japan Yasushi Misawa wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo vya usafi.
Mstahiki Meya Songoro Mnyonge akizungumza na wadau baada ya usafi.
Mstahiki Meya Songoro Mnyonge akizungumza na wadau baada ya usafi.Mkurugenzi Mkuu wa TCC Pic Takashi Araki akizungumza baada ya usafi. Balozi wa Japan hapa nchini Yusushi Misawaakizungumza.Mwenyekiti wa Bodi TCC Makanza akizungumza.
Mstahiki Meya akimpongeza Balozi Misawa.
Mstahiki Meya akizungumza jambo na Balozi Misawa.
Picha ya kumbukumbu.
Baadhi ya Wafanyakazi wa TCC
Picha ya kumbukumbu.
Picha ya kumbukumbu.
Wadau wakikabidhiwa vifaa ya kuhifadhia taka.
Msaanii George Sixtus Mdemu maarufu kwa jina la G Nako akitumbuiza baada ya usafi.
Viajana wakicheza wimbo wa G Nako.
Balozi Misawa na Mkurugenzi Mkuu TCC
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇