LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 22, 2024

DK. MAJULE AHAMASISHA WANAWAKE KUJITOKEZA KUGOMBEA UONGOZI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

 

Mwenyekiti wa  Umoja wa Wanawake  CCM (UWT), Mkoa wa Dodoma, Neema Majule akiongozana na wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji wamefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Chamwino mkoani humo.

Lengo la ziara hiyo iliyofanywa katika Kata ya Makang'wa ilikuwa ni;kuhuisha uhai wa CCM na  jumuiya hiyo, kuhamasissha ulipaji wa ada ya uanachama na ufanyaji wa vikao,  usajili wa wanachama kwenye mfumo wa kielektroniki, maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji pamoja na kuhamasissha  wanawake kugombea nafasi za uenyekiti wa vijiji, vitongoji  na ujumbe wa halmashauri za vijiji.

Malengo mengine yalikuwa ni; Kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi katika uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura shughuli itakayoanza mkoani humo Septemba 25 hadi Oktoba Mosi 2024,  Uandikishaji Wapiga Kura kwenye Daftari la Makazi  utakaoanza Oktoba 11 hadi 20, 2024 na kuwahamasisha vijana kujiunga na CCM.

Dk. Majule akiwa la Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Chamwino, Eveline Ndallu.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Chamwino, Eveline Ndallu.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma, Dk. Neema Majule

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI
BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages