LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 24, 2024

DK. KIKWETE AFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI MKUU WA GRENADA

Rais Mstaafu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Elimu la Kimataifa (GPE) amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Dickon Mitchell, Waziri Mkuu wa Grenada, Jijini New York, Marekani. 

Katika mazungumzo yao, Mwenyekiti wa GPE ameahidi kushirikiana na Visiwa vya Grenada ili kupatia ufumbuzi hitaji la elimu kwa njia ya mtandao (digital learning) ambalo taifa hilo linahitaji kuwezesha upatikanaji wake kwa wanafunzi wa elimu msingi (basic education) yaani, chekechea, msingi na sekondari.

Rais Mstaafu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete  akizungumza na Dickon Mitchell, Waziri Mkuu wa Grenada, Jijini New York, Marekani. 
Wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo.
 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages