LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 23, 2024

DK. BITEKO, MAHAKAMA WAFANYA MAZUNGUMZA NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA VIETNAM, LEO

Na Bashir Nkoromo, CCM's Officia. Blog
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amesema Tanzania na Vietnam zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu na zinaendelea kuuimarisha uhusiano huo katika nyanja za diplomasia, siasa na uchumi.

Amesema hayo wakati akizungumza na Ujumbe wa viongozi waandamizi 12 wa Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) ukiongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho (CPV), Phan Dinh Trac, katika Ukumbi wa Wizara ya Nishati Jijini Dar es Salaam,  leo Septemba 23, 2024.

Katika mazungumzo hayo pia ameipongeza Vietnam kwa kufanya uwekezaji nchini Tanzania ikiwemo katika Kampuni ya Simu za Halotel na kusema kuwa nchi hizo zinahitaji kuongeza kiwango cha biashara kati yake ambapo kiwango cha uwekezaji kwa sasa ni dola za kimarekani milioni 300.

Kwa upande wake, Trac ameipongeza Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuvutia uwekezaji, kuboresha huduma za afya, sanjari na kupiga vita vitendo vya rushwa.

Ameongeza kuwa, kufuatia jitihada hizo kiwango cha ukuaji uchumi kwa mwaka nchini Tanzania kimefikia asilimia 6.5 na kuwa Tanzania ina mchango mkubwa kwa maendeleo ya Afrika na dunia kwa ujumla na kuahidi kuwa  nchi yake itaendelea kushirikiana na kuimarisha uhusiano wake na Tanzania uliodumu kwa takribani miaka 60 huku akiiombaTanzania kuwa kiunganishi kati ya Vietnam na Umoja wa Afrika katika nyanja mbalimbali za maendeleo.

Mapema kabla ya kukutana na Dk. Biteko, Trac na Ujumbe wake walitembelea kwanza Mahakama ya Tanzania na kufanya mazungumzo na viongozi wakuu waandamizi wa mahakama, katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Temeke, Dar es Salaam.

Trac alifanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Elisante Ole Gabriel na Jaji Dk. Angelo Rumisha ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Maboresho, ambapo waliwaeleza viongozi hao wa CPV historia ya mahakama nchini Tanzania na mabadiliko ya kimaendeleo yaliyofanyika na yanayoendelea kufanywa kwa lengo la kuhakikisha utoaji wa haki unaendelea kuimarika nchini.

Kwa upande wake, Trac alishukuru kwa kupata fursa ya kujifunza  namna mahakama ya Tanzania inavyofanyakazi na kuwapongeza kwa mafanikio yaliyopatikana huku akisema mazingira ya utendaji kazi wa mahakama ya Tanzania hayana tofauti kubwa na yale ya nchini kwao.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko akizungumza na Mjumbe wa kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam Phan Dinh Trac (kulia), katika Ukumbi wa Wizara ya Nishati Jijini Dar es Salaam,  leo Septemba 23, 2024.

Dk. Biteko akimfurahia mgeni wake (Trac), baada ya kuingia ukumbini.
Dk. Biteko akisalimiana na Trac kabla ya kuketi kwa ajili ya kuanza mazungumzo. Kulia ni Balozi wa Vietnam hapa nchini Vu Thanh Huyen.
Mazungumzo yakiendelea.

Trac akimpa zawadi ya Picha ya Chuo Kikuu cha Vietnam Dk. Biteko.
Dk. Biteko akimpa zawadi ya korosho zilizofungashwa mgeni wake, Trac.
Dk. Biteko akiwa katika picha ya pamoja na Trec pamoja na Wajumbe waadamizi walioshiriki mazungumzo.

 

Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Elisante Ole Gabriel  akimueleza Trac na ujumbe wake historia ya mahakama nchini Tanzania na mabadiliko ya kimaendeleo yaliyofanyika na yanayoendelea kufanywa kwa lengo la kuhakikisha utoaji wa haki unaendelea kuimarika nchini.

Trac (kushoto) akiwa kwenye mazungumzo na Viongozi Wakuu Waandamizi wa Mahakama.
Ole Gabriel  na Trace wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe waandamizi walioshiriki mazungumzo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages