LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 23, 2024

DK. KIKWETE ASHIRIKI 'SIKU YA MAJI' YA MKUTANO WA SAYANSI JIJINI NEW YORK

 Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Wadhifa wake wa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kimataifa inayojishughulisha na Masuala ya Maji Barani Afrika (Global Water Partnership - Southern Africa and Africa Coordination Unit - (GWPSA - Africa) ameshiriki katika “Siku ya Maji” ya Mkutano wa Sayansi uliofanyika pembezoni mwa Mkutano wa 79 wa Umoja wa Mataifa, Jijini New York, Marekani. 


Katika Mkutano huu, Rais Mstaafu ametoa wito kwa nchi za Afrika na wadau mbalimbali duniani, kuendelea kuwekeza katika Mpango wa Maji wa Afrika unaolenga kuboresha upatikanaji wa maji safi, salama na toshelevu barani Afrika.




No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages