LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 7, 2024

CCM KUWEKEZA KWENYE MIRADI YENYE TIJA


 

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesisitiza kuendelea kuwekeza katika miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile barabara, elimu, na maji, ili kuhakikisha wananchi wengi wanapata maendeleo kupitia juhudi za serikali. Akizungumza katika Halmashauri ya Msalala, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, John Mongela, alisema kuwa hatua hizi tayari zimeleta matunda, hasa kupitia huduma bora za afya ambazo zimeboresha maisha ya wananchi.


Mongela aliongeza kuwa serikali imekamilisha mchakato wa kumpata mkandarasi wa mradi wa barabara kutoka wilaya ya Kahama kuelekea Kakola, barabara ya kilometa 73 inayounganisha mkoa wa Geita, ambayo inatarajiwa kuimarisha uchumi wa mikoa hiyo miwili.


Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mboni Mhita, alisema zaidi ya shilingi bilioni 100 zitatumika katika mradi huo wa barabara, ambazo ni sehemu ya maono ya Rais Samia Suluhu Hassan.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages