LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 8, 2024

KAMATI YA UWT KUENDESHA KAMPENI YA UTOAJI MSAADA WA KISHERIA- KATIMBA


 Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Haki na Sheria ya Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania (UWT), Zainab Katimba amesema kuwa UWT ina mpango wa kuanzisha Kanzi Data ya Mawakili Wanawake watakaokuwa wanatoa msaada wa kisheria nchini. 

 Akielezea mikakati ya kamati hiyo, Katimba amesema wataweka utaratibu wa mawakili hao pamoja na washirika wao wa kutoa huduma ya msaada wa kisheria kila wiki ya mwisho ya mwezi katika mikoa mbalimbali nchini kwa lengo la kuwafikia walengwa zaidi.IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages