LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 4, 2024

MASHAMSHAMYATAWALA MAPOKEZI YA DK NCHIMBI KIGOMA


Vikundi mbalimbali vikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel Nchimbi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma asubuhi hii , tayari kuanza ziara ya siku mbili mkoani humo

                                     .................................

Balozi DK Emmanuel Nchimbi anaanza leo ziara ya mikoa mitano ya Kigoma, Geita, Kagera, Mara na Mwanza 

Ameanzia leo Mkoa wa Kigoma ambapo pamoja na mambo mengine leo jioni atahutubia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Kigoma.

Alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma amelakiwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali wa mkoa huo  huku vikundi mbalimbali vikitoa burudani.

Baada ya kumaliza ziara ya siku mbili katika Mkoa huo ataendelea katika mikoa mingine minne ambayo ni Geita, Kagera, Mara na Mwanza.


Lengo la ziara hiyo ni; Kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020, kuhuisha uhai wa chama, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhakiki Taarifa zao na kujiandikisha katika kitabu Cha kudumu Cha Wapiga kura, kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba mwaka huu.


Katika ziara hii Dk Nchimbi ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Amos Makalla, Katibu wa NEC-Organaizesheni Ndg. Issa Ussi Haji (Gavu) pamoja na Katibu wa NEC- Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Rabia Abdallah Hamid.

Hivi karibuni amemaliza ziara ya siku nne yenye mafanikio makubwa katika mikoa ya Mtwara na Lindi.










 

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI
BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages