Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi DK Emmanuel Nchimbi anaanza leo ziara ya mikoa mitano ya Kigoma, Geita, Kagera, Mara na Mwanza
Ataanzia katika Mkoa wa Kigoma ambapo pamoja na mambo mengine leo jioni atahutubia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Kigoma.
Baada ya kumaliza ziara ya siku tatu katika Mkoa huo ataendelea katika mikoa mingine minne ambayo ni Geita, Kagera, Mara na Mwanza.
Lengo la ziara hiyo ni; Kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020, kuhuisha uhai wa chama, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhakiki Taarifa zao na kujiandikisha katika kitabu Cha kudumu Cha Wapiga kura, kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba mwaka huu.
Katika ziara hii Dk Nchimbi ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Amos Makalla, Katibu wa NEC-Organaizesheni Ndg. Issa Ussi Haji (Gavu) pamoja na Katibu wa NEC- Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Rabia Abdallah Hamid.
Hivi karibuni amemaliza ziara ya siku nne yenye mafanikio makubwa katika mikoa ya Mtwara na Lindi.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
0754264203


No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇