LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 4, 2024

MAPOKEZI YA DK NCHIMBI KIGOMA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma Tayri kuanza ziara ya siku mbili katika mkoa huo.

 Amelakiwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali wa mkoa huo  huku vikundi mbalimbali vikitoa burudani.

'.....................................

Balozi DK Emmanuel Nchimbi anaanza leo ziara ya mikoa mitano ya Kigoma, Geita, Kagera, Mara na Mwanza 


Ameanzia leo Mkoa wa Kigoma ambapo pamoja na mambo mengine leo jioni atahutubia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Kigoma.



Baada ya kumaliza ziara ya siku mbili katika Mkoa huo ataendelea katika mikoa mingine minne ambayo ni Geita, Kagera, Mara na Mwanza.


Lengo la ziara hiyo ni; Kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020, kuhuisha uhai wa chama, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhakiki Taarifa zao na kujiandikisha katika kitabu Cha kudumu Cha Wapiga kura, kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba mwaka huu.


Katika ziara hii Dk Nchimbi ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Amos Makalla, Katibu wa NEC-Organaizesheni Ndg. Issa Ussi Haji (Gavu) pamoja na Katibu wa NEC- Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Rabia Abdallah Hamid.

Hivi karibuni amemaliza ziara ya siku nne yenye mafanikio makubwa katika mikoa ya Mtwara na Lindi.

Dk Nchimbi akizungumza na wananchi waliofika kumlaki.
Katibu wa NEC-Organaizesheni Ndg. Issa Ussi Haji (Gavu) akijitambulisha kwa wananchi.

Dk Nchimbi akizungumza na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla.
Akizungumza na Katibu wa Oganaizesheni, Issa Ussi Haji Gavu.



Akisalimiana na baadhi ya viongozi waliofika kumlaki




 
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA

MHARIRI

BLOG YA TAIFA YA CCM

0754264203

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages