Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi, Dk. Emmanuel Nchimbi akipokea kadi za wanachama wa vyama vya upinzani walioamua kujiunga na CCM wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Community Centre Kigoma Mjini Agosti 4, 2024.
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla ametangaza kwenye mkutano huo kuwa hadi sasa CCM imevuna 5000 kutoka vya vyama vya upinzani katika mikoa 13 waliyofanya ziara, ambapo katika Mkoa wa Kigoma ambao ni wa 14 wamepokea wapinzani 200 miongoni mwao akiwemo aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kupita Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoka mkoa huo, Saprina Sungura na Diwani Patrick Wilizi wa Chama Cha Democratic (DP).
.................
Akimpokea Diwani Patrick Wilizi
Saprina Sungura akitaja moja ya sababu zilizomfanya ajiunge na CCM kuwa ni kupendezewa na utendaji wa Rais Samia Suluhu Hassan wa kuwaletea maendeleo watanzania ikiwemo Mkoa wa Kigoma.
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla akiwatangaza wapinzani waliojiunga na CCM.
Katibu wa Oganaizesheni, Issa Ussi Haji (Gavu) akiwapongeza wananchi wa Mkoa wa Kigoma kujitokeza kwa wingi kuhakiki na kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika zoezi lililofanyika mkoani humo hivi karibuni. Amewataka wote waliojiandikisha kujitokeza kwa wingi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba, 2024.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇