LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 23, 2024

DIWANI MANISPAA YA KINONDONI AIPONGEZA SERIKALI YA AWAMU YA SITA KWA KUUKAMILISHA MRADI WA DARAJA LA MAGUFULI MWANZA

Mwanza, leo.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mheshimiwa Songoro Mnyonge,  ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita, kwa kuuendeleza na kuukamilisha mradi wa ujenzi wa daraja la Magufuli linalounganisha Busisi na Kigongo, mkoani Mwanza.


Mheshimiwa Songoro alitoa pongezi hizoLeo Agosti 23,2024,  wakati wa ziara ya Waheshimiwa Madiwani na baadhi ya Watendaji wa Manispaa ya Kinondoni yenye lengo la kubadilishana uzoefu katika Usimamizi wa Miradi, usafi wa miji, uwezeshaji makundi maalum na ukusanyaji mapato.


Ziara hiyo inafanyika katika Jiji la Mwanza ambapo pia ameelezea haja ya kuanzisha ushirikiano baina ya Halmashauri hizo mbili.


Akiwa katika mradi huo wa daraja, Mheshimiwa Songoro alisema kuwa, "Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kutekeleza mradi huo vizuri. Huu ni mradi wa kitaifa, Sisi tumekuja kujionea ili tuweze kuusemea Kwa wananchi namna Serikali inavyoutekeleza."


Daraja hilo linatarajiwa kukamilika Disemba 30, 2024 ili lianze kutumika ambapo pamoja na kuunganisha mikoa ya Kanda ya Ziwa na Magharibi, pia litaiunganisha Tanzania na nchi za ukanda wa Maziwa Makuu. 

Matukio mbalimbali ya ziara hiyo👇




No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages