LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 7, 2024

BALOZI NCHIMBI ALAKIWA RASMI MKOANI KAGERA


Katibu Mkuu wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi akikagua gwaride la Umoja wa Vijana wa CCM baada ya kuvishwa skafu alipowasili mjini Biharamulo kuhudhuria mkutano wa ndani wa viongozi wa CCM wa wailaya hiyo Agosti 7, 2024, ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kikazi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. 

Kabla ya kuingia mkoa huo, amefanya ziara ya siku nne mkoani Kigoma. Dk Nchimbi tangu aingie madarakani ameshafanya ziara katika mikoa 14 na Kagera ni wa 15.

Katika mikoa hiyo amesikiliza zaidi ya kero 1000 za wananchi na kuzitatua. Pia amepokea zaidi ya wapinzani 5000 waliovihama vyama vyao na kujiunga CCM.

Malengo ya ziara hiyo ni; Kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020, kuhuisha uhai wa chama, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhakiki taarifa zao na kujiandikisha katika Kitabu cha Kudumu cha Wapiga kura, kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba mwaka huu.

Balozi Dk. Nchimbi, kwenye hiyo  ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) - Oganaizesheni, Issa Haji Usi Gavu, Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Rabia Hamid Abdallah,


Akiwasalimia viongozi wa CCM alipoingia katika mkutano huo wa ndani.
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mfunzo, CPA Amos Makalla akiongoza mkutano huo kwa kuwatambulisha baadhi ya viongozi walioambatana na Katibu Mkuu.

Dk. Nchimbi akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa.

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Kagera, Oliver Semuguruka akitambulishwa.



 IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA-0754264203

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages