Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi DK. Emmanuel Nchimbi na msafara wake kutinga Wilaya Ngara mkoani Kagera utakakofanyika mkutano mkubwa wa hadhara.
Asubuhi hii kabla ya kwenda Ngara atafanya mkutano wa ndani na viongozi mbalimbali wa CCM wa wilaya ya Biharamulo.
DK Nchimbi Jana alihitimisha ziara yake mkoani Kigoma kwa kuwasalimia wananchi Wilaya ya Kibondo, Kakonko na hatimaye kuingia Mkoa wa Kagera kwa kuwasalimia wananchi eneo la Nyakanazi wilayani Biharamulo.
Baada ya Dk Nchimbi kumaliza ziara Kagera ataendelea na ziara katika mikoa mingine ya Kanda ya Ziwa ambayo ni; Geita, Mara na Mwanza.
Malengo ya ziara hiyo ni; Kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020, kuhuisha uhai wa chama, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhakiki taarifa zao na kujiandikisha katika Kitabu cha Kudumu cha Wapiga kura, kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba mwaka huu.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇