LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 25, 2024

BABA HALISI AMSHUKURU RAIS DK. SAMIA KANISA HALISI KUSAJILIWA, AONGOZA SHEREHE YA UZINDUZI WA HUDUMA YA KANISA HILO, LEO

Na Bashir Nkoromo, CCM Official Blog, Tegeta
Baba Halisi Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa serikali anayoongoza kulipa usajili Kanisa hilo.

Pia amelishukuru Jeshi la Polisi kwa kuimarisha ulinzi na usalama, katika eneo la Kanisa hilo, kwa kufanya doria za mara kwa mara hata Kanisa lisipoomba kufanyiwa hivyo.

Baba Halisi ametoa shukurani hizo wakati akihubiri katika Sherehe ya Uzinduzi wa Huduma ya Kanisa Halisi, iliyofanyika Kao Kuu la Kanisa hilo, Tegeta Namanga, Jijini Dar es Salaam, leo Jumapili Agosti 25, 2024 au Lango la 12 Ethenimu 1, Majira Halisi kwa Kalenda ya Kanisa hilo.

"Naomba kumshuru mbele yenu Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassani kwa serikali yake anayoingoza kukubali kulisajili Kanisa hili, maana bila ridhaa yake kama kiongozi wa nchi angetaka angekataa tusisajiliwe, lakini kwa upendo na busara yake ameruhusu.

Pia, nalishukuru jeshi la Polisi kwa kutupatia ulinzi na pia kuwashukuru wananchi wa eneo hili (Tegeta Namanga) kwa kutupenda. Wakati tunaanza miaka saba iliyopita, hapa tulikuwa hatuna jengo kubwa, vifaa vyetu vya muziki vilikuwa vinalala nje, lakini hakuna hata waya ulioibwa", akasema Baba Halisi.

Katika sherehe hiyo mbali na Watekeleza Sauti (Wakuu wa vituo vya Kanisa Halisi) wa ndani na nje ya Tanzania, walihudhuria pia Kamanda wa Polisi Kinondoni ACP Mtatiro Kitinkwi, Baraza la Wazee mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo Mohamed Mtulia na Viongozi mbalimbali wakiwemo wa Kiislam na Kikristo.


Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi, Baba Halisi akiongoza Sherehe ya Uzinduzi wa Huduma ya Kanisa Halisi, Makao Makuu ya Kanisa hilo Tegeta Namanga Jijini Dar es Salaam,
leo Jumapili Agosti 25, 2024 au Lango la 12 Ethenimu 1, Majira Halisi.

Waimbaji wa Sauti Moja Halisi wakitumbuiza kuchangamsha maelfu ya waliohudhuria, mwanzoni mwa Sherehe hiyo.

Uzao (waumini) wakiserebula kwa furaha kumtukuza Chanzo Halisi.

Baba Halisi akiongoza kuinua shukurani mwanzoni mwa sherehe hiyo. Mama Halisi akipokea shukurani hiyo. Kulia ni Mnara Mmoja Halisi. Dk. Uelewa na Kanisa wake, wakipokea shukurani. Kulia ni Kamanda Mtatiro na Wazee wa Baraza la Wazee mkoa wa Dar es Salaam. Uzao na watekeleza sauti wakitoa matunda ya kupokea shukurani.

Mwimbaji akiongoza wimbo wa kumtukuza Chanzo Halisi.


Watekeleza sauti na Uzao wakifurahia wimbo huo wa kumtukuza Chanzo Halisi.
Uzao wakifurahia wimbo wa kumtukuza Chanzo Halisi.
Baba Halisi akieleza Huduma ya Kanisa Halisi zilizoanzia hadi zilipo sasa.
Baba Halisi akamtaja Dk. Uelewa na Kanisa wake walivyopokea Kanisa Halisi licha ya kuwa  Maprofesa wa Elimu ya Juu.
Dk. Uelewa Halisi na Kanisa wake wakasimama baada ya kutajwa na Baba Halisi.

Baba Halisi akieleza safari yake ilivyokuwa ya hatua ngumu ili aweze kuwa anapokea Sauti ya Chanzo Halisi badala ya kupokea ya shetani. Hapa amewainua Mama Halisi na Watoto waiotokana na Mama Halisi, wakati akifafanua zaidi.

Uzao wakiwa wametulia kumsikiliza Baba Halisi.

Waalikwa wakimsikiliza Baba Halisi.



Baba Halisi akifafanua kwa kina hatua mbalimbali kuhusu huduma ya Kanisa Halisi na zilivyopatikana kwa Sauti baada ya Majira saba.
Mtekeleza sauti akisoma kitabu kusasisha mahubiri ya Baba Halisi.
Waimbaji wa Sauti Moja Halisi wakiimba kutumbuiza ili Uzao watekeleza sauti waweze kupokea yaliyoachiliwa na Baba Halisi.
Uzao wakiburudika kwa wimbo huo.
Kamanda Mtatiro akizungumza baada ya kukaribishwa na Baba Halisi.
Baba Halisi akimpa mkono Kamanda Mtatiro kwa mawaidha mazuri aliyotoa.
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam Mzee Mtulia akikaribishwa na Baba Halisi kuzungumza jukwaani.
Mzee Mtulia akizungumza.
Baba Halisi akifurahi baada ya kupokea bahasha yenye ujumbe kutoka kwa Katibu wa Baraza hilo.
Baba Halisi akiongoza shukurani kufunga sherehe hiyo baada ya waalikwa mbalimbali kuzungumza.
Uzao na walikwa wakaanza kunywa soda ya sherehe hiyo.





Sherehe ikahitimishwa kwa waalikwa kuona bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wajasiriamali ambao ni Uzao wa Kanisa Halsi, kutekeleza Ibada ni Uzalishaji.

TAFADHALI SIKILIZA SHEREHE HIYO ILIPOKUWA MBASHARA HAPO👇

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages