LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 30, 2024

ZIARA YA BALOZI DK. NCHIMBI KUSINI YAFYEKA CHADEMA, ACT NA CUF

Mpilipili, Lindi Mjini

Ziara ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, mikoa ya Mtwara na Lindi, imevifyeka vyama vya upinzani kufuatia viongozi waandamizi wa vyama vya ACT Wazalendo, CUF na Chadema na mamia ya wanachama wa vyama hivyo kutimkia CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Lindi, leo.


Pamoja na kutimkia CCM viongozi waandamizi na wanachama wa vyama hivyo walirejesha kadi zao za vyama vya vyao kwa Balozi Dk. Nchimbi kwa kasi kubwa kwenye mkutano huo. 


Katika mkutano huo uliofanyika Uwanja wa Mpilipili, viongozi waandamizi waliopokewa na Balozi Nchimbu ni pamoja na Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo Mkoa wa Lindi, Mbunge Mstaafu wa Mchinga Hamidu Bobali na  Mwenyekiti wa Wanawake ACT Wazalendo Lindi Mjini Hawa Kipara.



Wengine ni Meneja Kampeni wa Wabunge ACT Wazalendo Lindi, aliyekuwa Mwenyekiti wa Vijana CUF Lindi Issa Sapanga, Katibu wa ACT Wazalendo Mkoa wa Pwani, Mwenyekiti wa Chadema Mchinga, Mwenyekiti wa Wanawake Chadema Lindi Mjini na Wanachama 250 wa ACT Wazalendo.


 “Nimeishi miaka 20 nje ya CCM ambako niliaminiwa sana katika ngazi tofauti ndani ya CUF na ACT Wazalendo hadi kuwa Waziri Kivuli wa Maji lakini nikiri niliyokuwa nayapigania Jemedari Samia ameyafanya kwa nguvu kubwa hivyo sina jinsi isipokuwa kujiunga CCM na kumuunga mkono. 


Kule upande wa pili tulikokuwa ametupiga kwenye mshono, hakuna tena agenda. Sasa hakuna kingine zaidi ya kazi nzuri za Dk. Samia na wenzangu hawa sasa tupo tayari kumsaidia." amesema Babali wakati akikabidhi kadi ya ACT na kujiunga CCM.


Akiwapokea Balozi Dk. Nchimbi wanachama hao wa vyama mbalimbali wakiongozwa na ACT Wazalendo amesema  “karibuni huku wanachama wote ni sawa na mtapata ushirikiano mkubwa sana kuanzia sasa na kikubwa mmesema mmerudi sababu ya mambo makubwa yaliyofanywa na Dk. Samia, nawapongeza kwa kuliona hilo mapema sasa tukaifanye Lindi ya kijani.






No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages