LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 30, 2024

CCM YASAFISHA UPINZANI LINDI, MAMIA WAHAMIA CCM


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi akipokea kadi za wanachama wa Chama cha ACT Wazalendo, Chama Cha Wananchi (CUF) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliohamia CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mpilipili  mjini Lindi Julai 30, 2024. Zaidi ya wanachama 250 na viongozi wa vyama hivyo wamehamia CCM.

Viongozi hao wameongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Lindi na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Mchinga, Hamidu Bobali akiambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Wanawake wa ACT Wazalendo Lindi Mjini Bi. Hawa Kipara, Meneja Kampeni wa Wabunge ACT Wazalendo Lindi na aliyekuwa Mwenyekiti wa Vijana CUF Lindi Issa Sapanga, Katibu wa ACT Wazalendo Mkoa wa Pwani, Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Mchinga, Mwenyekiti wa Wanawake Chadema Lindi Mjini.

Akizungumza baada ya kukabidhi kadi na nyaraka zingine, Bobali amesema kuwa; “Nimeishi miaka 20 nje ya CCM ambako niliaminiwa sana katika ngazi tofauti ndani ya CUF na ACT Wazalendo hadi kuwa Waziri Kivuli wa Maji lakini nikiri niliyokuwa yanapigania, Jemedari Samia ameyafanya kwa nguvu kubwa hivyo sina jinsi isipokuwa kujiunga CCM na kumuunga mkono. Kule upande wa pili tulikokuwa ametupiga kwenye mshono, hakuna tena agenda.”

Balozi Nchimbi akiwapokea wanachama hao amewapongeza  kwa uamuzi wao wa kuhamia CCM na  kuwaahidi kuwapatia  ushirikiano mkubwa sana hasa baada ya kuukubali muziki wa Rais Samia katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Lindi.


 Dk Nchimbi akimkaribisha CCM aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Mkoa wa Lindi, Hamidu Bobali baada ya kutangaza kuhamia chama hico kutokana na kufurahishwa na utendaji mzuri wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, CPA Amos Makalla akionesha bendera ya ACT wazalendo.
Katibu wa Siasa na Mambo ya Nje wa CCM, Rabia Abdala Hamid akionesha furaha baada ya CCM kuwapokea wapinzania hao.

Mbunge wa Mchinga, Salma Kikwete akiwa na furaha alipokuwa akiwapokea wanawake wa upinzani waliohamia CCM.


Waliokuwa wanachama wa vyama vya upinzani wakionesha kadi za vyama hivyo kabla ya kukabidhi kwa Katibu Mkuu, Dkt Nchimbi.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA

MHARIRI

BLOG YA TAIFA YA CCM

0754264203


No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages