LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 31, 2024

USHINDI WA CCM UNATOKANA NA MTAJI WA WANACHAMA WAKE- MTATURU.

 




MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amesema ushindi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),katika chaguzi zijazo utatokana na mtaji wa wanachama uliopo na sio vinginevyo.

Mtaturu ametoa kauli hiyo Julai 29,2024,wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Kikio Kijiji cha Munane akiwa kwenye ziara yake ya kutoa mrejesho wa Bunge la Bajeti 2024/2025,kuhamasisha uchaguzi wa serikali za mitaa,vijiji na vitongoji 2024 na kusikiliza kero za wananchi.



Amesema mbali na uwepo wa mtaji wa wananchama,pia upo mtaji wa wananchi wenye mapenzi na CCM.

"Nipo hapa kujibu maneno yaliyokuja kuzungumzwa hapa kwamba CCM inashinda kwa kusaidiwa hapana,ushindi wa CCM unatokana na mtaji wa wanachama wake,lakini wapo watu ambao hawana chama lakini wanaipenda CCM na wanaipa kura na wengine wapo walio vyama vingine lakini kutokana na kazi nzuri inayofanywa na serikali ya CCM akifika kwenye sanduku la kura anaweka ndio kwa CCM hili linapaswa lieleweke,"amesema.

Ziara ya Mtaturu jimboni humo inamfikisha katika kila Kijiji akibeba jumbe tatu ambapo ziara hiyo ameipa jina ya Kishindo Jimboni Kijiji kwa Kijiji.



 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages