LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 29, 2024

WANAWAKE WAGALAGALA CHINI KUONESHA FURAHA YA KUMLAKI DK NCHIMBI

Wanawake wakiglagala chini ikiwa ni ishara wenyeji wa eneo la Mingoyo kuonesha  furaha ya kumlaki Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel Nchimbi alipowasili eneo hilo akitokea mkoani Mtwara tayari kwa mapokezi ya kuanza ziara mkoani Lindi Julai 29, 2024.


Akiwa katika hilo, Dk Nchimbi alisikiliza na kuzitatua kero za wananchi ikiwemo upatikanaji wa eneo la kuegesha malori, bei ndogo ya korosho.

Lengo la ziara hiyo ni; Kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020, kuhuisha uhai wa chama, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhakiki Taarifa zao na kujiandikisha katika kitabu Cha kudumu Cha Wapiga kura, kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba mwaka huu.


Katika ziara hii Dk Nchimbi ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Amosi Makalla, Katibu wa NEC-Organaizesheni Ndg. Issa Ussi Haji (Gavu) pamoja na Katibu wa NEC- Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Rabia Abdallah Hamid.



 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages