Wananchi wakifurahia hotuba makini ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).Dk Emmanuel Nchimbi alipokuwa akihutubia katika vijiji vya Mpapula Mtwara na Mingoyo Lindi akiwa katika ziara ya kikazi katika mikoa hiyo.Julai 29, 2024.
Lengo la ziara hiyo ni; Kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020, kuhuisha uhai wa chama, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhakiki Taarifa zao na kujiandikisha katika kitabu Cha kudumu Cha Wapiga kura, kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba mwaka huu.
Katika ziara hii Dk Nchimbi ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Amosi Makalla, Katibu wa NEC-Organaizesheni Ndg. Issa Ussi Haji (Gavu) pamoja na Katibu wa NEC- Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Rabia Abdallah Hamid.
Mbunge wa Nanyamba, Abdallah Chikota akiwa amefurahishwa na hotuba ya Dk Nchimbi
Mbunge wa Mtwara Mjini, Hassan Mtenga akishangilia.
Kwaya ikitumbuiza
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI
BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203













No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇