LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 29, 2024

DK NCHIMBI KUTINGA LINDI LEO

 


 Ziara ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Balozi, Dk. Emmanuel Nchimbi inaingia leo Mkoa wa Lindi baada ya kumaliza katika Mkoa wa Mtwara.

Kabla ya Katibu Mkuu kuondoka Mtwara atakuwa na kikao cha ndani na Kamati ya Siasa ya Mkoa.

Baada ya hapo Katibu Mkuu na msafara wake ataelekea Mtwara Vijijini, ambapo atakuwa na mkutano wa kusalimia wananchi eneo la Mpapura. 


Kutoka hapo msafara wake utaelekea Mkoa wa Lindi kwa kusimama Kata ya Mnonela Jimbo la Mtama, kusalimia wananchi, kisha baadae atasalimia wananchi Kata ya Mingoyo, kisha utaelekea Lindi mjini. 


Lengo la ziara hiyo ni; Kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020, kuhuisha uhai wa chama, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhakiki Taarifa zao na kujiandikisha katika kitabu Cha kudumu Cha Wapiga kura, kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba mwaka huu.


Katika ziara hii Dk Nchimbi ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Amosi Makalla, Katibu wa NEC-Organaizesheni Ndg. Issa Ussi Haji (Gavu) pamoja na Katibu wa NEC- Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Rabia Abdallah Hamid.



No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages