Taasisi ya Maendeleo ya Kijamii ya Wananchi, LEKIDEA (Legho Kirua Vunjo Development Asociation) ni taasisi ya kupigiwa mfano hapa nchini.Hayo yalisemwa na kubainishwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, Mhe Zainab Katimba katika kikao na watendaji wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini-TARURA na Wajumbe wa LEKIDEA ofisini kwake Jijini Dodoma hivi karibuni kuzungumzia ujenzi wa barabara inayojengwa kwa ubia kati ya TARURA na LEKIDEA kutoka Uchira hadi kwa Laria kupitia Shule ya Sekondari Kisomachi yenye urefu wa km 10.9.
Naibu Waziri Katimba aliyasema hayo baada ya kusikiliza hoja iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa ujumbe wa LEKIDEA Eng.Saimon Njau kuhusu kasi ndogo ya ujenzi wa barabara hiyo ambayo makubaliano ya TARURA na LEKIDEA yalifanyika mwaka 2019.
Katika mazungumzo hayo Ujumbe wa LEKIDEA ambao uliongozana na Mbunge wa Vunjo, Dkt. Charles Kimei, Diwani wa Kata ya Kirua Vunjo Mashariki Mhe. Alex Umbela, Mwenyekiti wa wajumbe Eng Saimon Njau,Mwenyekiti wa Taasisi Bw.Edward Fabian Msaki akiongozana na katibu wake Joseph Shewiyo pamoja na wajumbe wengine washika dau wa maendeleo.
Wakati upande wa Serikali Naibu Naziri Mhe.Zainab Katimba (ambaye alimwakilisha Mhe. Waziri Mwenye dhamana na TAMISEMI) katika kikao hicho ambacho TARURA iliwakilishwa na Mkurugenzi wa Barabara Vicent Komba akimwakilisha Mtendaji Mkuu TARURA Eng.Gilibert Mwoga ambaye ni Mkurugenzi wa miundo mbinu TAMISEMI.
Watendaji walieleza sababu za kutotekeleza kwa wakati kuwa kulikuwa na changamoto la ugonjwa wa COVID na uhaba wa fedha na kuwa mwaka huu wametenga shilingi milioni 750 kutengeneza kilometa 0.8 na mwaka 2024/25 shilingi milioni 500 kutengeneza kilometa 1.0.
Mheshimiwa Naibu Waziri Mhe.Zainab Katimba baada ya kusikiliza pande zote mbili na kuwapongeza wana LEKIDEA kwa moyo wa kujitolea kushirikiana na Serikali kujenga barabara; aliahidi kwa kushirikiana na Mbunge wa Vunjo Dkt.Charles Kimei swala hilo watalifikisha kwa Mhe. Waziri anayesimamia TAMISEMI.
Mradi huu wa ujenzi wa Barabara hii ya Uchira kwa Laria kupitia Kisomachi ulianza baada ya kufanyiwa upembuzi yakinifu kati ya uongozi wa Kata,LEKIDEA na TARURA na kuingia mkataba wa kisheria.
LEKIDEA kama taasisi ya wananchi na Mshika Dau wa Maendeleo ya jamii ilikubaliana na TARURA kuchangia pipa za lami 299 na shilingi milioni mia mbili (Tsh. 200,000,000/= )
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa wajumbe wa LEKIDEA Eng Simon Njau LEKIDEA taasisi ya kijamii yenye wanachama wasiozidi 300 wadau wa maendeleo ya jamii wa Kata ya Kirua Vunjo Mashariki iliyopo mkoani Kilimanjaro Wilaya ya Moshi Vijijini.
Taasisi ya LEKIDEA ikishirikiana na Wananchi wa Kata ya Kirua Vunjo Mashariki inayoundwa na vijji vya Mero,Kileuo,Lasso,Mrumeni na Nganjoni baada ya ubia na TARURA iliyopo chini ya TAMISEMI Kujenga barabara yenye urefu wa zaidi ya kilometa 10 kuanzia Uchira hadi kwa Laria kupita Shule ya Sekondari Kisomachi na Soko laTaifa (Gulio la kuuza mazao mbali mbali ya wananchi wa Kata ya Kirua Vunjo Mashariki)
Katika mradi huu wa Barabara ya Uchira hadi kwa Laria LEKIDEA wameshatoa pipa zote za lami kama waliyo ahidi katika makubaliano yaoi na TARURA. –
Mapipa ya lami tayari yapo eneo la mradi.Pia kukabidhi mchango wa Fedha Shilingi milioni mia moja na thelathini (Tsh.130,000,000/=)sehemu ya malipo ya makubaliano ya LEKIDEA kuchangia ujenzi wa Bara bara hii.
Mwenyekiti huyo alibainisha kuwa pamoja na kuchangia nguvu kubwa katika ujenzi wa Barabara wanashirikiana na wananchi katika mambo mbalimbali ya kijamii- kimaendeleo Kama:utunzaji wa mazingira na upandaji miti,ujenzi wa nyumba ya ibada na Kituo cha afya.
Ndani ya Kata hii kuna taasisi kadhaa zilizo wafanya Wana-Lekidea kujipanga na kuunda Umoja wa kushirikiana na wananchi wa eneo hili hasa katika Swala zima la Miundo Mbinu mibovu ya Bara bara zilizokuwa hazipitiki hasa kipindi cha mvua.
Baadhi ya Taasisi zilizopo katika Kata hii ya Kirua Vunjo Mashariki ambazo ni wanufaika wakubwa wa Taasisi hii ni:
Shule ya Sekondari Kisomachi,Shule ya Sekondari Kilimani,Shule ya Sekondari Uchira,Shule ya Msingi Lasso,Shule ya Msingi Legho,Shule ya Msingi Mrumeni,Shule y msingi Msufini,Chama cha Ushirikia Kirua Vunjo Mashariki KNCU, pamoja na Taasisi za kidini yakiwamo makanisa kadhaa,Kanisa la Karumeli na Legho Kilema pamoja na Soko la mazao ya kilimo-Taifa lililopo Kisomachi Kisomach penye ofisi ya Kata na ofisi;ofis ya Kijiji cha Kileuo nani njia panda inayounganisha vijiji vyote vinavyounda Kata ya Kirua Vunjo Mashariki.
Taasisi iliona umuhimu kuungainsha wadau wa maendeleo wanaotoka Kata ya Kirua Vunjo Masharikii kukusanya nguvu pamoja na kushirikiana na wananchi wanao ishi Kata hii kusukuma Maendeleo mbele Bila kujali tofauti za kiitikadi.
Taasisi ya LEKIDEA pamoja na kuelekea nguvu nyingi kwenye miundo Mbinu korofi ya Barabara za Kata ya Kirua Vunjo Mashariki pia imeelekeza nguvu katika swala la kuhifadhi na kutunzamazingira
Kwa mujibu wa Katibu na Mratibu wa LEKIDEA Ndugu Joseph Shewiyo Taasisi ya LEKIDEA kwa kushirikiana na wananchi wameshaotesha miche ya miti elfu 30 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 90 .Kila mche uligarimu wastani wa shilingi elfu 3 kununua, kusafirisha hadi ugawaji miche kwa walengwa vijijini.
Taasisi hii inautaratibu wa kuotesha miche ya miti zaidi ya elfu tano kila Mwaka; huwa inanunua miche na kuigawa bure kwa wananchi-jamiii.
Pia taasisi inautaratibu wa kukarabati Barabara za ndani ya vijiji hasa zile sehemu korofi ili ziweze kupitika nyakati zote za Mwaka.
Taasisi hii ya LEKIDEA Pia imenunua eneo la ardhi lenye thamani ya milioni 30 lenye ukubwa wa zaidi ya hekari tano kwaajili ya ujenzi wa kituo cha afya .
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇