LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 10, 2024

KIONGOZI MKIMBIZA MWENGE WA UHURU KITAIFA AMPONGEZA RAIS DK. SAMIA KUBORESHA ZA WATANZANIA


 

Na HEMEDI MUNGA, Mkalama 


KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka huu, Godfrey Mnzava amempongeza na kumshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoendelea kupambania  tiba za watanzania.


Mnzava ametoa pongezi hizo wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru ulipofika katika hospitali ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida, kuangalia vifaatiba vilivyowezeshwa na Rais Dk. Samia.


"Mheshimiwa Rais Dk. Samia ameendelea kujenga miundombinu mingi sana ambayo ni  rafiki na  yakisasa kutolea huduma za afya," amesema.


Ameeleza miundombinu hiyo ni pamoja na Zahanati, vituo vya afya, hospitali za wilaya,  mikoa na kanda ikiwemo kuimarisha hospitali ya Taifa.


Amedokeza  Rais ameyafanya hayo kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kibingwa na hawapati changamoto ya kuzifuata mbali na makazi yao.


Amebainisha kua mbali ya kuendelea kuboresha maslahi ya watumishi, lakini ameendelea kuleta vifaatiba na dawa.


"Ameleta vifaa ambavyo vinasaidia kutafsiri changamoto za wagonjwa na mifumo ya hewa tiba kwa lengo la kuwasaidia watu wenye changamoto ya kupumua na upatikanaji wa hewa ndani ya miili yao ili waweze kupata unafuu," amesema.


Amebainisha hayo yote, yanaonesha namna Raia Dk. Samia anavyoangaikia afya na uzima wa watanzania kwa lengo la kuhakikisha wanaendelea kua na afya bora na kuendelea kutoa mchango wao kwa Taifa.


Amesema Rais ameleta fedha nyingi kwa lengo la kuhakikisha mifumo hiyo inakaa vema na kufanya kazi vizuri.


"Hapa pia mmeletewa vifaa hivyo, tumekagua na kuona namna ambavyo vinaendelea kufanya kazi, kwa kweli tunampongeza na kumshukuru  sana Rais Dk. Samia Suluhu Hassan," ameshukuru.


Katika hatua nyingine, Mnzava amewataka wataalam wa afya kuendelea kuvitunza vifaa hivyo kwa lengo la kuhakikisha vinatoa huduma kwa muda mrefu kwa viwango na ubora unaostahiki.


Hatua hiyo, inawezesha kuendelea kuwahudumia wananchi waliopo hivi sasa na wale watakaokuja baadae.


Awali akiwasilisha taarifa fupi ya vifaa vya kisasa walivyovipata, Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya hiyo, Nicas Leonart amesema wanamshukuru Rais kwa kuwapatia vifaa ambavyo wanaamini vitawanufaisha wananchi.



Aidha, ameeleza serikali iliwapatia fedha za  kujenga jengo la wagonjwa wa dharura kupitia mradi wa mapambano ya UVIKO-19 mwaka 2021.


Amesema mradi huo, uligharimu sh millioni 300 kutoka serikali kuu huku katika mwaka 2023 hadi 2024 wakipokea  vifaatiba vyenye thamani ya sh milioni 450.5.


Daktari Leonart amevitaja vifaa hivyo kuwa ni Portable x-ray, Oxygen Port, ventilators, Control ya Mfumo wa hewa tiba, Maniford Control (Mfumu wa hewa tiba), vitanda vya umeme vitano na vifaa vingine.


"Vifaa hivi lengo lake ni kuboresha huduma kwa wagonjwa wa dharura," amesisitiza.


Hata hivyo, Leonart ameweka wazi  mradi huo, utawanufaisha wananchi wilayani humo ikwemo wilaya za jirani za Meatu, Iramba na Mbulu.


"Tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha nyingi," ameshukuru.


Mwenge wa Uhuru umekimbizwa wilayani hapa umbali wa  kilometa 79 wakati hadi kuufikisha wilaya ya Singida  zitakua zimetimia kilometa 134.




Picha zote na Hemedi Munga.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages