LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 10, 2024

DC MWENDA AMKABIDHI DC MACHALI MWENGE WA UHURU




 Na HEMEDI MUNGA, Mkalama 

Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida, Suleiman Mwenda amemkabidhi  Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Mkalama,  Moses Machali Mkoani hapa.


DC Mwenda amekabidhi  Mwenge huo wa Uhuru leo katika kijiji cha Msingi kata ya Msingi  wilayani Mkalama  baada ya kuulinda na kuukimbiza kilometa 68.1 ukiwa unawaka, unangaa na kumeremeta kwa muda wote ulipokuwepo Iramba.


Aidha, ameweka wazi kuwa ulitembelea,  kuona, kuweka mawe ya msingi, kupata taarifa mbalimbali ikiwemo kuizindua miradi saba yenye  thamani ya sh bilioni 5.084 ambazo zilitolewa na serikali anayoiongoza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.


"Hakika tunaendelea kumshukuru  Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, tunaomba ndugu Kiongozi Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Godfrey Mnzava utufikishie salam kwake  na tunamuahidi mitano tena ifikapo 2025 tukianza na uchaguzi huu wa serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu," ameahidi DC Mwenda.




No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages