MBUNGE wa Njombe Mjini, Deo Mwanyika akiwa katika ziara Kata ya Kifanya amewapongeza wananchi wa vijiji vya Kifanya, Utengule na Lwangu kwa kuchangia na kuendeleza shughuli mbalimbali za ujenzi katika vijiji vyao kama ujenzi wa shule shikizi kitongoji cha ITENGULE - KIFANYA, shule shikizi MZALENDO - LWANGU na ujenzi wa nyumba ya Mtendaji kijiji cha UTENGULE.
Mhe. Mwanyika
amewachangia tripu 10 za mawe ujenzi wa shule shikizi ITENGULE zenye thamani ya
Sh. 1,300,000, saruji mifuko 30 (Sh. 555,000) ujenzi wa nyumba ya Mtendaji
Kijiji cha Utengule, saruji mifuko 20 (Sh. 370,000) ujenzi wa shule shikizi
Mzalendo - Lwangu. Chanzo cha fedha:- Fedha binafsi.
Pia tenki la
maji shule ya Msingi Msindu lenye thamani ya (Sh.
2,000,000) na saruji mifuko 30 (Sh. 555,000) shule shikizi Mzalendo
- Lwangu zitatolewa kupitia Mfuko wa jimbo.
Mwanyika amewaasa
wananchi kuendelea na moyo ya kuchangia shughuli mbalimbali za
maendeleo na serikali itaendelea kutoa fedha katika ujenzi huo.
Serikali imeendelea kuunga mkono juhudi za wananchi kwa kutoa fedha katika
Sekta ya Elimu, Afya, Kilimo, Maji, Barabara na Umeme ikiwa lengo kuu ni
kumsogezea huduma bora mwananchi katika maeneo yao.
Mwanyika ameanza ziara
jimboni kwake yenye lengo la kukagua miradi ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji
wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020, kusikiliza na
kutatua kero za wananchi, kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kuhakiki
taarifa zao kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa ajili ya maandalizi ya kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba mwaka huu, pamoja na kuhuisha uhai wa
chama.
#Njombe mpya,
#Dira mpya, kazi
iendeleee
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇