LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 21, 2024

MGANE, MBUNGE LUGANGIRA WAMSHUKURU RAIS SAMIA KUWALEA WATOTO 6





Tarehe 11/7/2024 Mhe Neema Lugangira ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu, alipokea wito kutoka kwa Rosemary Stanslaus wa kufika Mtaa wa Nyakanyasi, Kata ya Bakoba, Bukoba Mjini kuangalia namna ya kumsaidia Makarius Sypirian Mgane mwenye watoto 6 wadogo. 

Tarehe 13/7/2024 Lugangira kushirikiana na Dada Rebecca, Afisa Ustawi wa Jamii Kagera walikabidhi msaada wa  magodoro, vyandarua, blanketi na vyombo. Lugangira na Mgane wameshukuru Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwachukua watoto hao sita na kuwapeleka kwenye vituo vya kulelea.

"Hakika, Baba huyu anastahili pongezi na msaada, yeye ni mfano wa baba bora; na kupitia picha hizi ambazo baba ameridhia Mhe Neema Lugangira anaomba tumuongezee tabasamu kupitia #NeemaNaMaendeleoFund" Lugangira

 IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI
BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages