LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 26, 2024

WAFUGAJI ZAIDI YA 3000 NCHINI KUKUTANA KWENYE KONGAMANO LAO JULAI 28 IGUNGA


NA VICTOR MAKINDA. IGUNGA TABORA.

Zaidi  ya wafugaji 3000 na wadau wengine wa sekta hiyo hiyo,  kutoka maeneo mbali mbali nchini, wanatarajia kukusanyika Wilayani Igunga mkoani Tabora kwa ajili ya kufanya Kongamano kubwa la kujadili mafanikio na changamoto zinazoikabili sekta hiyo.

Hayo yameelezwa leo mjini Igunga na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wafugaji Tanzania (CCWT) Ally Manonga (pichani)

Manonga amesema kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, imetatua matatizo mengi yaliyokuwa yakiikabili sekta ya ufugaji nchini, zipo changamoto chache zinazoikabili ambazo bado zinaikabili sekta hivyo hivyo kongamano hilo litajadili na kupendekeza utatuzi wa changamoto hizo.

"Matatizo mengi ya wafugaji yametatuliwa, bado yapo machache ambayo pia yanatakiwa kutupiwa jicho ili kuyapatia ufumbuzi wa kudumu". Amesema.

Manonga amesema kuwa kongamano hilo linalotarajiwa kufanyika tarehe  28.7.2024 litajadili mafanikio, changamoto na namna ya kutatua changamoto zilizosalia.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages