Na Oscar Assenga, Tanga
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewakaripia madereva wanaofanya shughuli za usafirishaji katika mkoa wa Tanga wanaojihusisha na vitendo kutoa rushwa wanapokamatwa na Polisi wa usalama kutokana na makosa mbalimbali ya kukiuka sheria za usalama barabarani.
Badala yake Chama kimewataka, badala ya kutoa rushwa madereva hao wahakikishe wanazingatia sheria na taratibu zote za usalama barabarani.
Karipio hilo limetolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo Rajabu Abdurhaman wakati akimetoa kwa niaba ya Chama Sh. Milioni 30 kugharamia masomo ya madereva 600 wa daladala katika Chuo cha VETA Jijini Tanga, waweze kukidhi vigezo vinavyotumika kuendesha vyombo vya usafiri.
“Pamoja na yote niwasisitize madereva kuhakikisha tunafuata sheria za usalama barabarani kwa kuendesha vyombo vyetu vya moto tukiwa tumekidhi vigezo kwa kuwa na leseni”Alisema
Mwenyekiti huyo pia aliwataka madereva hao kuacha kuendesha vyombo vya moto kiholela bila kufuata sheria za usalama barabarani kwani kufanya hivyo wanachangia kuhatarisha maisha yao na abiria ambao wanakuwa wamepanda kwenye vyombo vyao.
“Lakini niwatake pia msiwe mahodari wa kulaumu askari wa usalama barabarani kwa sababu wamekiuka sheria za usalama badala yake wafuate utaratibu ili amani iendelee kutawala wanapokuwa wakiendesha vyombo vya moto.”Alisema Mwenyekiti huyo
“Ninaamini baada ya kupata mafunzo haya kwa mwezi mmoja kwenye katika chuo cha Veta kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani yatawawezesha kuwaongezea elimu na kupata leseni ili kukidhi vigezo vya sheria vilivyowekwa”Alisema
Alisema lakini pia mafunzo hayo yatawaepusha na adha ya kukamatwa askari wa Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo ya kukosa leseni za udereva
Awali akizungumza katika halfa hiyo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian alimshukuru Mwenyekiti huyo kwa kuwasaidia madereva hao kuweza kupata elimu katika chuo cha Veta itakayowawezesha kupata vigezo vya kuendesha vyombo vya moto.
Alisema kwamba viongozi wa madereva hao walifika ofisini kwake wakimpelekea malalamiko ya kuwa wanapokuwa katika shughuli zao wanakamatwa na polisi leseni zao zinachukuliwa na magari yao kuwekwa kituo cha polisi na wao kuwekwa ndani kutokana na kukosekana ukamilifu wa viwango ambavyo vinatakiwa ya kila mwenye leseni wawe wamekwenda chuo na kupata cheti cha kusomea.
“Nilipopata jambo hilo lilinisikitisha kidogo nikaona njia ya kuwasaidia nikaone nije kwako Mwenyekiti wetu wa Mkoa wa CCM kukueleza kilio hicho na baadae ukaona uwaite wakakuelezea shida zao na wewe ukaamu kulifanyia kazi sisi wengi tunahaidi lakini ahadi zetu zinaweza kuchukua mwaka au mwezi umehaidi na ahaidi yako imetilia kwa wakati tunakushurku sana,” Alisema
“Mwenyekiti nikuhaidi kwamba tutaendelea kufanya kulingana na spidi yako na sisi kama serikali tutaiga kuhakikisha kila tunachokihaidia tunakitekeleza kwa wakati nah ii itapunguza kero na adha kubwa ambayo polisi walikuwa wakipata lakini madereva walikuwa wakipata na wengine kukosa ujira baada ya kukamatwa na gari kushikiliwa”Alisema
Naye kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Tanga (RTO) Inspekta Rajabu Ngumbi alisema kwamba kumekuwepo na idadi ya madereva ambao wamekuwa wakikamatwa kwa makosa ya kutokuwa na leseni ambalo ni suala muhimu kwao wanapokuwa barabarani.
Ngumbi alisema kwamba lazima madereva wahakikisha wanakidhi vigezo vya kuendesha vyombo vya moto kwa kuhakikisha wanapata elimu na baadae kukidhi kupata leseni ili kuweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.
MWENYEKITI
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman (kulia)
akimkabidhi Sh. milioni 30 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi
Dk. Batilda Burian kusaidia madereva wa 600 daladala kusoma Chuo cha Veta, jana. (katikati mwenyenye kofia) ni Mkuu
wa Chuo cha Veta Tanga.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇