LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 20, 2024

MBUNGE NJEZA AANZA ZIARA YA KIKAZI MBEYA VIJIJINI


 




 
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini, Oran Njeza  akiwa ziarani Kata ya Ikukwa amechangia sh 400,000 za chakula kwa wanafunzi wa shule mbili za msingi, laki 2 kwenda shule ya msingi Itende Juu na nyingine Shule ya Msingi Ikukwa.

 

Tangu aanze ziara za vijiji kwenye kata hiyo, Mhe. Njeza amewasisitiza wazazi kushiriki kikamilifu michango ya chakula kwa sababu wanafunzi wakipata chakula shuleni ufanisi, utimamu na utulivu utaongezeka na ufaulu utakuwa juu zaidi.

Njeza akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Simboya Kata ya Ikukwa ambapo amewapatia Sh. milioni 2 kwa ajili ya uendelevu wa ujenzi wa nyumba ya mganga wa Kituo cha Afya cha Ikukwa.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages