LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 24, 2024

RAIS DK. MWINYI AWAKANA WANAOTAKA AONGEZEWE MUDA, AWASIHI KUFUNGA MJADALA, ASEMA NI HOJA ISIYO NA TIJA KWA NCHI WALA KWA CCM, MAKALLA AKOMELEA MSUMARI

Na Bashir Nkoromo, Offcial CCM Blog
Ikulu ya  Zanzibar imesema maoni yanayopendekeza Rais Dk. Hussein Mwinyi aongezewe muda wa Urais kwa miaka saba badala ya mitano na kwamba Uchaguzi wa Mkuu wa mwakani wa Rais wa visiwa hivyo usifanyike ni jambo ambalo halina tija wala faida kwa nchi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) chenye kufuata misingi ya demokrasia.

"Rais Dk. Mwinyi ni muumini wa kufuata Katiba na Sheria za nchi, tunapenda kusisitiza kwamba maoni haya si ya Mhe. Rais wala sio ya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar.

Kwa muktadha huu, Rais Dk. Mwinyi anaendelea kuheshimu utaratibu uliowekwa wa Rais kuchaguliwa kila baada ya miaka mitano. Aidha, amewesihi wale wote wenye mawazo tofauti na hayo wafunge mjadala huo", imesema,Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Charles Hilary, leo Juni 24, 2024.

Wakati huohuo, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla amesema hoja ya kuongeza muda wa Urais kwa Rais wa Zanzibar, Dk. Mwinyi kutoka Miaka Mitano hadi 7, haipo

Akihojiwa na Clouds FM, leo, Makalla amesema jambo halipo, halijafika Halmashauri Kuu, CCM inaendeshwa na vikao, kikao cha Kamati Maalum Zanzibar halijafika.

Rais Dk. Hussein Mwinyi

TAARIA YA IKULU ZANZIBAR👇


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages