LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 8, 2024

RAIS DK. SAMIA ATOA WITO SEKTA BINAFSI KUONGEZA UWEKEZAJI NA UPATIKANAJI WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Na Bashir Nkoromo, Official CCM Blog, JNICC
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ametoa mwito kwa sekta binafsi nchini kuongeza uwekezaji na upatikanaji wa nishati safi ya kupikia katika maenep mbalimbali nchini.

Sanjari na mwito huo, Rais amewataka kuleta teknolojia rahisi itakayowezesha wananchi kupata nishati safi kadri ya uwezo wao pamoja na kulipia kulingana na matumizi kama inavyofanyika katika huduma ya umeme.

Rais amesema hayo katika hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati safi ya Kupikia wa Mwaka 2024-2034 iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam, leo Aprili 8, 2024.

Amesema Mkakati huo unatoa mwongozo wa Kitaifa kwa wadau wote kuhakikisha nchi inafikia leongo ililojiwekea la silimia 80 ya Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

Rais amesisitiza kuwa lengo la Mkakati huo likitekelezwa  na kutimia litapunguza gharama ya nishati safi ya kupikia na kuongeza upatikanaji na uwekezaji wa nishati safi.

Amebainisha kuwa Mkakati huo wa Kitaifa pia utachangia jitihada za Serikali za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabaianchi kutopkana na uharibifu wa misiti ambao huchangiwa na shughuli za binadamu.

"Kwa sasa inakadiriwa takriban hekta 469,000 za misitu kupotea kila mwaka, nishati za kuni na mkaa ni moja ya chanzo kikuu cha kutoweka misitu hiyo",  amesema Rais Dk. Samia.

Rais amesema hivi sasa asilimia 90 ya Watanzania wanatumia nishati ambayo si salama kwa afya zao, hiyo
ili Mkakati huo ufanikiwe, Serikali inalojukumu la kuwaelimisha wananchi kwa namna mbalimbali kuhusu umuhimu wa kutumia nishati safi ya kupikia.

“Tuachane na utamaduni wa sasa, tubadilike kifikra na kwenda kwenye utamaduni mpya ili kuwezesha watu wengi kutumia nishati safi, ambayo ni salama kwa afya na mazingira yetu.” amefafanua.

Uzinduzi huo pia umehudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Dotto Biteko, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dk. Suleiman Jaffo, Spika wa Bunge na Rais wa Bunge la IPU Dkt. Tulia Ackson, Mawaziri na Manaibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya, pamoja na wadau wa mazingira na wananchi mbalimbali.

Rais Dk. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati safi ya Kupikia wa Mwaka 2024-2034 iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam, leo Aprili 8, 2024.
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa Mkakati wa Matumizi wa Nishati Safi ya Kupikia wakati wa hafla ya uiznduzi huo iliyofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, leo Mei 8, 2024. Pamoja naye ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (Wapili kushoto), Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Dotto Biteko (kulia) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dk. Suleiman Jaffo.
Rais Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwenye hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam
Rais Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwenye hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam
Rais Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dk. Suleiman Jaffo Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwenye hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.
Rais Dk. Samia akimkabdhi Waziri wa Maji, Nishati na Madini wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Shaib Hassan Kaduara
Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwenye hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.
Rais Dk. Samia akiongoza viongozi na wananchi kusimama wakati wimbo wa taifa ukipogwa waati wa hafla hiyo.
Ras Dk. Samia akimsikiliza kwamakini Naibu Waziri Mkuu, Waziri wa Nishati Dk. Biteko wakati wa hafla hiyo.
Waalikwa na washiriki mbalimbali wakiwe kwenye hafla hiyo.
Waalikwa na washiriki mbalimbali wakiwe kwenye hafla hiyo.
Waalikwa na washiriki mbalimbali wakiwe kwenye hafla hiyo.
Waalikwa na washiriki mbalimbali wakiwe kwenye hafla hiyo.
Waalikwa na washiriki mbalimbali wakiwe kwenye hafla hiyo.
Waalikwa na washiriki mbalimbali wakiwe kwenye hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages