LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 29, 2024

Chalamila: Nitafanya kampeni hadharani wazembe wasipitishwe CCM

Ibrahim Bakari, Oficial CCM Blog 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema atafanya kampeni za waziwazi na hadharani kwenye Kamati ya Siasa ya Mkoa ili viongozi wazembe wasipitishwe. Akizungumza na wakazi wa kata mbalimbali za Pugu wakati wa kusikiliza kero za wananchi kwenye Uwanja wa Pugu Kajiungeni Mei 28, 2024,


 Chalamila amesema amejitolea muhanga kuwaharibia wale wote wazembe watakaoomba kutetea nafasi zao. Amesema endapo atakuwepo mkoani, ataingia kwenye Kamati za Siasa za Mkoa za kupitisha wagombea kwenda kuwaharibia wale wote wazembe kwamba hawakufanya chochote, wezi, wazembe na hawafai kurudishwa. Amesema wanatakiwa viongozi walionyooka wa kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan kutekeleza majukumu yake kwa kutatua kero za wananchi.. Akikazia mwaka wa uchaguzi, amesema ataanzia kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu, wenyeviti wote walioshindwa kuwajibika hawana sababu ya kurudi, awe CCM au chama chochote. Huku madiwani na watendaji wakimsikiliza kwa makini, amewaagiza wananchi kuwapiga chini kuanzia watendaji wa mitaa, wabunge na madiwani bila kupepesa wala kuona aibu. Chalamila amesema akibahatika kuwepo hadi 2025, atakuwa balozi wa kampeni ya kudondosha Mjumbe wa Mitaa, Diwani hata Mbunge kwamba arudi au asirudi kutokana na kile walichofanya. Amewataka wanaofanya uteuzi, kuhakikisha wanapata watu makini kwa ajili ya kutatua kero za wananchi kwa kuwa CCM ina watu wengi makini na wachapa kazi. Akimzungumzia Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Slaa ambako mikutano umefanyika, amesema kuwa amemwambia atashangaa kusikia wananchi wa jimbo hilo hawalali kwa migogoro ya ardhi. Aidha amesema kuwa atamshangaa Slaa kulalamika hana barabara wakati Bungeni anakaa na mawaziri wenye dhamana ya kutengeneza barabara na akamwambia kuwa Bunge likimalizika ataweka kambi kushughulikiwa matatizo yote jimboni. Kuhusu dampo la Kinyamwezi, amesema pamoja na kwamba inaelezwa kujaa, bado nafasi ipo ya kuendelea kumwaga taka.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages