LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 29, 2024

BALOZI DK. NCHIMBI AWATAKA WANANCHI KUDUMISHA UMOJA NA MSHIKAMANO


Hemedi Munga, Ikungi, Singida
 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi amewaomba wananchi wa Kata ya Isuna Jimbo la Singida Mashariki kwa kushirikiana na Watanzania wengine kuendelea kujenga umoja miongoni mwao.
 
 Dk. Nchimbi ametoa kauli hiyo wakati aliposimama kusalimia wananchi hao akiwa katika ziara yake mkoani Singida aliyoianza Mei 29, 2024.
 
 Akizungumza na maelfu ya wananchi hao, Dk. Nchimbi amewataka kuhakikisha hawabaguani kwa misingi ya kabila, rangi, itikadi za vyama au upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
 "Mkimuona Mtanzania yeyote anaanza kuwabagua watu kwa misingi ya kabila, dini au upande ambao mtu anatoka katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnatakiwa kumkataa mtu wa namna hiyo," amesema.
 
 Aidha, amewafahamisha watu wenye tabia ya namna hiyo wanaweza kuwa msingi wa kuigawa nchi yao, kuifarakanisha na kuleta vita katika nchi.
 
 "Hatuwezi kukubali nchi yetu ifike huko, Chama cha Mapinduzi na Wanachama wake wakiwemo Watanzania lazima waungane kukataa kuigawa nchi yetu na kuwafarakanisha Watanzania kwa namna yoyote ile," amesisitiza.
 
 Pia, amewaomba washirikiane na kuahidi kushirikiana kufanya watoto wao wanarithi nchi nzuri kama walivyorithi wao. Amesema ni dharau kubwa kwa wazazi wao ikiwa watawakabidhi watoto wao nchi iliyoharibika.
 
 Ameweka wazi wazazi wao wamefanya kazi kubwa kuwapatia nchi nzuri yenye umoja na mshikamano. "Namna pekee ya kuwaheshimu wazazi wetu ni kujenga nchi yenye umoja kama walivyo tukabidhi, tuhakikishe tunalinda utulivu, umoja na mshikamano wetu kwa nguvu zetu zote," amesisitiza.
 
 Aidha, amebainisha CCM haitaacha kuendelea kuwasisitiza Watanzania pasina kuchoka kuwa nchi hii ni yao, hivyo wanawajibu wa kuilinda na kuitetea.
 
 Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama hicho mkoa huo, Martha Mlata amemuhakikishia Balozi Dk. Nchimbi kuwa wananchi wamejitokeza na kufurika kila walipo simama na kufanya mkutano kwa lengo la kutoa shukurani kwa Rais Dk. Samia kwa mambo makubwa ambayo yamefanyika katika mkoa huo.
 
 "Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) umefanyika vizuri, ninakuomba umpelekee salamu Rais wetu Dk. Samia Suluhu Hassan mwambie tunamshukuru sana kwa upendo wake na kwanamna alivyojitoa kuwahudumia wananchi," ameomba. 
 
 Naye Mkuu wa Mkoa huo, Halima Dendego amesema wanamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuwapa Rais Dk. Samia kwa sababu mkono wake Wanasingida wameuona. 
 Ameweka wazi katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake, mkoa huo ulipokea takribani sh trilion 1.7 kwa lengo la kutekeleza shughuli za serikali na miradi ya maendeleo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Singida, Martha Mlata akimuahidi Katibu Mkuu wa Chama hicho, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi kumuonesha Rais Dk. Samia Suluhu Hassan upendo wao katika masanduku ya kura kwa zaidi ya  asimia 100, wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani manyoni mkoani hapa. (Picha na Hemedi Munga)

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego akimshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuupa mkoa huo fedha nyingi kutekeleza miradi ya maendeleo, katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Manyoni mkoani Singida. (Picha na Hemedi Munga)

Wananchi mbalimbli wa wilaya ya Ikungi wakiwa katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, uliofanyiaka Puma wilayani Ikungi mkoani hapa. (Picha na Hemedi Munga)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages