LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 21, 2024

MBUNGE RWEIKIZA AFANYA MAKUBWA JIMBONI KWAKE


Na Lydia Lugakila,

Bukoba


Mbunge wa Jimbo la Bukoba vijijini Jasson Rweikiza, ameanza ujenzi wa Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Bukoba vijijini ambayo itagharimu shilingi Milioni 150.


Taarifa ya ujenzi wa ofisi ya CCM katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba  imetolewa April 21,2024 Wakati akizungumza na Wananchi waliotaka kujua ufafanuzi wa Ujenzi huo na utekelezaji wa wake umefikia wapi.


"Nikweli CCM Bukoba vijijini hatukuwa na Ofisi ya Chama hivyo niliona nianze ujenzi mara moja kwa kugharamikie kila kitu ili tuweze kupata Ofisi yetu na tayari ujenzi umeishaanza na umefikia hatua nzuri na tunakamilisha mwaka huu tumetumia gharama kubwa katika kusafiri kila wakati kwenda Bukoba mjini kufanya vikao na shughuli za chama kiwilaya sasa itakuwa mwisho"amesema Rweikiza


Rweikiza alisema ujenzi wa Ofisi umefikia asilimia 60 uko hatua ya kuezeka, ambapo katika jengo hilo kuna ofisi mbalimbali ikiwemo ya UVCCM, UWT, Jumuiya ya Wazazi, Ofisi ya Mwenyekiti, katibu wa Wilaya na Tehama pamoja na ukumbi ambao utakuwa na uwezo wa kuhudumia zaidi ya watu 200 kwa wakati mmoja.


Aidha Katibu wa Siasa  uenezi na mafunzo CCM Wilaya Bukoba vijijini Deokras Byabato alisema kuwa  Mbunge Rweikiza anajenga Ofisi hiyo kwa niaba ya Chama na dhamana aliyopewa  kwa sababu ilikuwa ni muhimu wao kuwa na Ofisi ili kuondokana na changamoto ya kutumia ofisi za kuazima wakati shughuli za chama na ujenzi vilianza  mwezi June mwaka jana na utakamilika mwishoni mwa mwaka huu.


"Mbunge wetu amejitolea kujenga Ofisi ambayo sisi kama chama tulikuomba atusaidie kufanya hivyo kwasababu tulikuwa tunapata changamoto kubwa hasa kwenye shughuli za Chama kwa kusafiri kufuata majengo ya Serikali Bukoba mjini jambo ambalo lilikuwa ni changamoto kwetu Ila kwa sasa tunaona changamoto inakwenda kuisha"alimesema Byabato


Naye Philipina Atelius mkazi wa Kijiji katoju kata Bujugo Halmashauri ya Bukoba na Mjumbe wa Kamati ya ujenzi wa Ofisi hiyo ya CCM alisema halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ilikipatia Chama na kiwanja chenye na ukubwa wa heka 10 katika Mtaa wa Bujunangoma  kata Kemondo karibu na ofisi za halmashauri ambapo wanaamini watapata huduma zote  ili kuwezesha ujenzi wa Ofisi hiyo.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages