LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 22, 2024

DK. NCHIMBI: CCM TUTAENDELEA KUMUENZI KAPTENI KOMBA


 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Mkurugenzi wa Tanzania One Theatre (TOT) ya CCM,  marehemu Kapteni John Komba alipozuru kaburi hilo katika Kata ya Lituhi, wilayani Nyasa Mkoa wa Ruvuma wakti wa ziara ya kikazi Aprili 21, 2024.

Katika tukio hilo aliambatana na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, Katibu wa Oganaizesheni, Issa Haji Gavu na Katibu wa Idara ya Uchumi na Fedha, Dk Frank Hawasi.

Dkt Nchimbi amesema kuwa CCM itaendelea kumuenzi marehemu Dkt Komba kwa mambo mazuri aliyoifanyia chama hicho na kuhakikisha hayapotei.


Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla akiweka shada la maua kwenye kaburi hilo ikiwa ni ishara ya kumuenzi.

Katibu wa Oganaizesheni, Issa Haji Gavu akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa msanii wa chama hicho na Mkurugenzi wa TOT.


Katibu wa Idara ya Uchumi na Fedha, Dkt Frank Hawasi akiweka shada la maua.
Dkt Nchimbi na viongozi wengine wa chama hicho wakitoa heshima walipozuru kaburi hilo.
Dkt Nchimbi akitoa neno la kumuenzi aliyekuwa jabal ya kutunga nyimbo murwa za hamasa za chama.

 George Komba ambaye ni Mtoto wa Marehemu Komba akitoa shukrani kwa Dkt Nchimbi kuzuru kaburi hilo na kuelezea kuwa moja ya mambo aliyowausia babao kuwa muda wote wawe karibu na chama hicho na kuhakikisha kinashinda katika chaguzi zijazo,


IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA

0754264203

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages